28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI WAWILI WAFUKUZWA KAZI MWANZA

Na CLARA MATIMO – MWANZA


JESHI la Polisi Mkoa wa Mwanza  limewafukuza kazi askari wake wawili kwa kukutwa na   vipande viwili vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 20.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna, aliwaambia waandishi wa habari   jana  kwamba askari hao   namba H 5461 PC Enock  wa kikosi cha kutuliza ghasia Mkoa wa Mwanza na H 4165 DC Robert, wa kikosi maalumu  walitenda kosa hilo Agosti 23 mwaka huu saa 10.00 jioni eneo la Nyamhong’olo Wilaya ya Ilemela.

Alisema   askari hao walikamatwa baada ya kupata  taarifa kutoka kwa raia wema kwamba walikuwapo watu waliokuwa wanajihusisha na biashara ya meno ya tembo ndipo walishirikiana na kikosi kazi cha taifa cha kupambana na ujangili kanda ya ziwa.

Alisema baada ya kuwakamata walifanya uchunguzi na kujiridhisha kwamba wamehusika na biashara hiyo hivyo Agosti 27 waliwafukuza kazi na muda wowote watawafikisha mahamamani baada ya uchunguzi kukamilika.

“Askari hao tumewafukuza kazi kutokana na kutenda kosa kinyume na mwenendo wa jeshi la polisi.

“Sasa naomba niwaambie wenzao wote ambao walikuwa wanashirikiana nao kufanya biashara hiyo wajisalimishe wenyewe katika kituo chochote cha polisi kilicho karibu nao.

“Vingenevyo watambue kwamba tutawakamata muda wowote tena nawapa saa chache  kuanzi sasa maana kama tumeweza kuwakamata askari wetu wao ni kama nzi hata kama wako nje ya nchi maana tunao askari wetu wa interpol hawatatushinda,” alisema Kamanda Shanna.

Alisema sheria ni msumeno unakata kotekote haiangalii sura, cheo elimu wala kabila la mtu, kwa hiyo yeyote atakayejuhusisha na uhalifu wa aina yoyote atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles