33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi wasimamia upigaji kura CCM

NA, MURUGWA  THOMAS, TABORA

JESHI la polisi juzi lililazimika kusimamia marudio ya kura  za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mtaa wa Kizigo Manisaa ya Tabora, baada ya makundi ya wagombea kutunishiana misuri.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya wanachama kugomea maelekezo yaliyotolewa na uongozi wa kata kwamba wanaoostahili kupiga kura ni wale wenye kadi na si vinginevyo.

Wapambe wa wagombea walikataa kufuata maelekezo hayo, huku wakidai waendelee na makubalino ya awali ambapo walipiga kura kwa kujiandikisha kupitia matawi kitendo ambacho kilidaiwa ni kukiuka katiba na kanuni za uchaguzi ndani ya chama hicho.

Kutokana na mvutano wa makundi ya wafuasi wa wagombea kuanzia saa 6 mchana, taarifa zilifika ngazi ya wilaya ambao nao walilazimika kumweleza Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Erick Komanya ambaye alifika eneo la uchaguzi akiwa ameambatana na askari wakiwa na  silaha za moto.

Wakizungumza na gazeti hili,  Thomas Mapesa   alisema kuchelewa upigaji kura kulisababishwa na uongozi wa CCM kata kuwazuia wanachama wasiokuwa na kadi kushiriki tofauti na walivyowatangazia.

‘’ Kura za maoni tulizopiga juzi hatukuambiwa kufika na kadi za chama, tunashangaa wanatulazimisha kuzileta ndiyo tupige kura,’’ alisema.

Alisema wanachama halali  walishajiunga muda mrefu walichokuwa wakisubiri ni kukabidhiwa kadi zao.

Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa Wilaya, Rashid Ramadhan aliyeifika eneo la uchaguzi akiwa na mkuu wa wilaya alisema waliamua kufuta matokeo ya awali baada ya kulalamikiwa na baadhi ya wagombea kutokana na kukiukwa kanuni za uchaguzi. Baada ya kurudiwa upigaji kura, Adam Bahati aliibuka tena mshindi kwa kupata kura 44 wakati uchaguzi wa awali alishinda kwa 216 kitendo ambacho kinadhihilisha wengi walioshiriki uchaguzi wa huo hawakuwa halali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles