26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi waliowacharaza wanafunzi wafukuzwa kazi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari

Na  PENDO FUNDISHA-MBEYA

JESHI la polisi mkoani Mbeya limewafukuza kazi  polisi wawili  kwa   kukiuka maadili ya kazi baada ya kuwafanyia vitendo vibaya wanafunzi wa kike wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Isuto  iliyopo Mbeya vijijini.

Askari hao ni PC Petro Mgana mwenye namba H 4925 wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Mbeya (FFU) na PC Lukas Ng’weina wa Wilaya ya Polisi Mbalizi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea November 15 usiku,   katika Shule ya Sekondari ya Isuto iliyopo Kijiji na Kata ya Isuto Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Polisi   Mbalizi.

Alisema inadaiwa   askari hao kwa pamoja wakiwa kwenye ulinzi wa mitihani ya taifa ya kidato cha nne ya mwaka huu,  waliwatoa kwenye hosteli wanafunzi wa kike kwa kile walichodai kuwa walikuwa wanapiga kelele.

“Baada ya kuwatoa wanafunzi hao nje, waliwapeleka eneo la foleni na kuwapa adhabu zikiwamo kupiga push up, kuruka kichura, kushika masikio na kuwachapa viboko,”alisema.

Alisema  adhabu hizo ziliwasababishia maumivu makali na baadhi yao kuondoka shuleni kurudi  nyumbani kwao.

“Baada ya vitendo hivyo, jeshi la polisi limewachukulia hatua za  nidhamu askari hao kwa kuwafukuza kazi kuanzia tarehe 08.11.2016 na baadaye watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika,”alisema.

Hata hivyo, habari zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kwamba  Magana  amelitumikia jeshi hilo kwa miezi minne tu tangu afuzu mafunzo yake katika Chuo Cha polisi Moshi (CCP) huku Lukas akiwa amekwisha kuilitumikia kwa miaka miwili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles