25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi wakamata wahamiaji 51

Gustaphu Haule ,Pwani

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani, limewakamata Wahamiaji haramu 51 waliokuwa wakiingia nchini kupitia bandari bubu ya Makurunge wilayani Bagamoyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,  Wankyo Nyigesa, alithibitisha kutokea tukio hilo.

Alisema wahamiaji hao, walikamatwa  saa 11 alfajiri Machi 19, mwaka huu.

Alisema watuhumiwa walikabidhiwa kwa vyombo vingine vya dola kwa taratibu za kisheria  ili wachukuliwe hatua.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zainabu Kawawa alisema wahamiaji hao walikutwa porini wakiwa katika harakati za kutafuta usafiri kwenda  mikoa ya nyanda za juu kusini ili kuendelea na safari ya kwenda Afrika Kusini.

Alisema walikuwa wanaotoka nchini Ethiopia, ambapo katika mahojiano ya awali walikiri kuingia nchini kupitia Pwani ya Bagamoyo wakitumia majahazi. 

Alisema walichukuliwa hadi kituo cha afya Matimbwa  ili kupimwa kama wana maambukizi ya virusi vya Corona, lakini majibu hayajatolewa.

“Wahamiaji wamefikishwa  kituo hiki ili kufanyiwa vipimo vya awali kujiridhisha kama hawana maambukizi ya ugonjwa wa corona,  kabla ya kupelekwa gereza la Kigongoni,wakisubiri kusomewa mashtaka yao,”alisema Kawawa

Wakati huo huo,jeshi hilo linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji,baadae kuzika mwili wa marehemu katika shamba la mahindi.

Kamanda Nyigesa, alisema watuhumiwa walikamatwa Machi 19, huko Kibindu wilayani Bagamoyo, wakituhumiwa kuua na kuzika mwili.

Alisema Machi 3,mwaka huu, saa 8 mchana,mtuhumiwa Chacha Machangu (27) alimfumania mke wake akiwa na mwanaume mwingine .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles