27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi Moshi: Ilikuwa ni lazima kuzuia msafara wa Lowassa

RPCNa Upendo Mosha, Mosha

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limetoa ufafanuzi kwa vyomba vya habari kuhusiana na uamuzi wake wa kuzuia msafara wa mgombea wa urais Chadema, Edward Lowassa, likisema kuwa lilifanya hivyo kutokana na wingi wa magari na pikipiki zilizokuwa zikimsindikiza.

Akizungumza na vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani, alisema msafara uliokuwa ukimsindikiza Lowassa kwenye mazishi ya aliyekuwa mwasisi wa Chama Cha Mapinduzi, Peter Kisumo, ulikuwa mkubwa hivyo eneo la msiba lisingeweza kustahimili ukubwa huo.

Alisema msafara huo ulikuwa na magari zaidi ya 70 na pikipiki zaidi ya 600, hivyo kutokana na hali ya eneo la msiba kuwa dogo lisingeweza kustahimili wingi wa magari, pikipiki na watu ukilinganisha na magari yaliyokwisha tangulia msibani.

“Nikiwa Usangi nilipigiwa simu na Mheshimiwa Mbatia na Mheshimiwa Ndesamburo wakidai msafara wao umezuiliwa kwenda mazishini na ndipo nilichukua jukumu la kufuatilia ili kujua tatizo ambapo Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Mwanga alinieleza kwamba msafara una magari mengi na pikipiki, hivyo usingeweza kukaa katika eneo la msiba,” alisema Kamanda Ngonyani.

Alisema baada ya kupata taarifa hiyo aliwaeleza viongozi hao kuwa wangeweza kupata fursa ya kwenda katika mazishi hayo isipokuwa magari, wasaidizi pamoja na walinzi wao, jambo ambalo viongozi hao walikataa na polisi kulazimika kuzuia msafara huo.

Alisema baada ya polisi kusimamia msimamo wao wa kutaka viongozi hao wasiende na watu wote, walizira kuhudhuria mazishi hayo ya Mzee Kisumo na kugeuza msafara huo kurudi Moshi mjini.

Pia Kamanda Ngonyani alikanusha taarifa zinazozagaa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa kamanda huyo aliongea na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa amemzuia Lowassa kwenda msibani baada ya kupewa maelekezo kutoka ngazi za juu.

Alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kwamba ni uwongo na uzushi na kutoa wito kwa vyombo vya habari kuhakikisha vinaripoti taarifa ambazo ni sahihi na ambazo hazitaweza kuleta uchochezi katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

 

WAPAMBE WA LOWASSA KUPIGWA BOMU LA MACHOZI

Akizungumzia hatua ya Jeshi la Polisi kuwapiga bomu la machozi wafuasi wa Lowassa, Kamanda huyo alisema walilazimika kuwatawanya wananchi kwa kutumia bomu la machozi kutokana wananchi kuhamasishwa kuhudhuria mkutano wa hadhara katika eneo la njiapanda ya Himo.

Alisema viongozi wa chama hicho walikuwa wakihamasisha wananchi kutoka na kuingia barabarani kwa ajili ya maadamano, jambo ambalo lilikuwa kinyume cha sheria kutokana na kwamba walikuwa hawana kibali cha kufanya hivyo.

“Polisi kweli waliwapiga mabomu ya machozi wananchi ambao walikuwa wakihamasishwa na viongozi wa Ukawa kufanya maadamano, jambo ambalo ni kinyume cha sheria kutokana na kwamba hawakuwa na kibali cha kufanya hivyo,” alisema Ngonyani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles