30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI HAINA TAARIFA ZA KUKAMATWA KWA ALIYESAMBAZA PICHA ZA NYUFA

Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam, limesema halina taarifa za kukamatwa kwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Kumbusho Dawson kwa tuhuma za kupiga picha hosteli mpya za chuo hicho (JPM) Block A, zinazoonyesha nyufa katika jengo hilo.

Awali, taarifa za kukamatwa kwa Kumbusho, zilithibitishwa na Waziri Mstaafu wa Mikopo chuoni hapo, Shitindi Venance ambaye alidai alipelekwa kupelekwa kituo Kikuu cha Polisi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema, jeshi lake bado halijapata taarifa kamili kuhusu tukio hilo na endapo watapata taarifa hizo na watazifanyia uchunguzi wa kina na kutatoa taarifa.

Wakati huo huo, Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), umesema baada ya ukaguzi wa wataalamu wao wamebaini nyufa hizo ni za kawaida katika taaluma ya wabunifu majengo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Elius Mwakalinga amesema kitaaluma majengo mapana huwekewa nafasi ambayo hutenganisha na kuwa sehemu mbili ambapo hali hiyo husaidia kuruhusu jengo kupumua inapotokea hitilafu ya udongo kutanuka na kusinyaa kutokana na hali ya hewa.

“Kutokea kwa nyufa katika jengo letu hili si kwa sababu ya upungufu wa ubunifu ujenzi bali umetokea katika maeneo yaliyokusudiwa na kitaaluma hutokea hivyo, hazina madhara,” amesema Mwakalinga.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles