31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Polisi, Chadema wapishana kukamatwa wasaidizi wa Mnyika

Na BENJAMIN MASESE-MWANZA

WAKATI Jeshi la Polisi likijitokeza hadharani na kusema kuwa hakuna  viongozi wa  Chadema waliotekwa mkoani humo isipokuwa walishikiliwa na polisi kwa mahojiano baada ya wananchi wa Kata ya Mahina kutoa taarifa kwamba si watu wema.

Pamoja na hali hiyo nacho Chadema kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje ya Nje wa chama hicho, John Mrema hiyo ya polisi inauposhaji kuhusu tukio hilo na sababu ya kukamatwa kwa maofisa hao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Murilo alisema taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wasaidizi wa Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika wametekwa si za kweli ambapo aliwataka wananchi kuzipuuza.

Alisema viongozi waliokuwa wameshikiliwa na polisi ni  Katibu wa Katibu Mkuu wa Chadema, Abdulkarim Muro (31) na dereva wake, Said Haidani (30), walikuwa mikononi kwa polisi tangu juzi saa 12 jioni baada ya raia wema kutoa taarifa polisi kwamba kuna watu wawili wanahisiwa si wema  na wamekuwa wanaingia katika nyumba moja iliyopo karibu na Hoteli ya Paradise.

Kamanda Murilo alisema baada ya taarifa hizo polisi walifuatilia kwa haraka na kufanikiwa kuwakamata na walipotakiwa kutoa maelezo ya awali ya utambulisho  waligoma na kulazimika kuwapeleka katika kituo kikuu cha polisi Mwanza kwa mahojiano zaidi.

“Walipofika  katika kituo kikuu cha polisi walikubali kutoa ushirikiano na kutoa vielelezo vyote na sababu ya kuwepo eneo lile, walisema wao ni wasaidizi wa Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na wapo pale kwa ajili ya kulala, hivyo baada ya polisi kujiridhisha tumewachia na wanaendelea na shughuli zao.

“Sisi kama jeshi la polisi  kazi yetu ni kuimarisha ulinzi kwa raia na mali zao, sasa inapotokea tumepata taarifa kutoka kwa raia wema tunaifanyia kazi haraka sana ndiyo maana tulifanya hivyo lakini kitendo ambacho kimetukera ni taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba wanachama wawili wa Chadema wametekwa,” alisema Murilo

Hata hivyo alipohojiwa sababu ya polisi tangu juzi  polisi walikuwa wanamfuatilia Mnyika wakiwa na gari za polisi na binafsi, Murilo alisema ni jukumu lao kuhakikisha kila raia anakuwa salama na mali zao hivyo hawezi kupangiwa namna ya kutimiza majukumu yao.

Pia alisema si kila kiongozi wa kitaifa anapaswa kulindwa na askari au kuongozwa na king’ora cha polisi, hivyo waliamua kumlinda Mnyika kwa namna wanavyojua wenyewe ilimradu tu awe salama.

KAULI YA CHADEMA 

Kutokana na hali hiyo alipotafutwa Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alipingana na taarifa ya polisi na kudai kuwa imepotosha kuhusu ukweli wa tukio hilo na sababu za kukamatwa kwa wasaidizi hao wa Mnyika.

“Hawa maofisa wetu wa chama na wako Mwanza na Katibu Mkuu (John Mnyika) kwa shughuli za kifamilia na mapumziko na walikamatwa wakiwa ndani ya eneo la Hoteli ya Paradise.

“Hivyo hatua ya polisi kueleza kwamba walikamatwa nyumba jirani na inabua hisia au jambo lilojificha katika tukio hili,” alisema Mrema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles