30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm apanga kuacha historia

yanga kochaNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Yanga, Hans van der Pluijm, amesema ataendelea kukisuka kikosi hicho kiendelee kuwa bora zaidi ili kama atakiacha na kuondoka aweze kufurahia mafanikio yake.

Katika kufanikisha mipango hiyo, kocha huyo raia wa Uholanzi amepanga kufanya usajili wa uhakika kwa ajili ya kujiimarisha zaidi na michuano ya kimataifa na Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Yanga msimu huu imepata mafanikio makubwa kwa kufanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii na kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA, huku ikifanya kweli kimataifa baada ya kuingia hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Pluijm ambaye ameipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo, amebakiza mwaka mmoja wa kuifundisha timu hiyo katika mkataba wake.

Akizungumza na MTANZANIA juzi kabla ya kuondoka kuelekea nchini Ghana, Pluijm alisema ili kufanikisha malengo yake ya kuifikisha mbali timu hiyo, amepanga kuelekeza nguvu kubwa kwenye usajili ili apate kikosi bora na imara zaidi.

“Hakuna kocha yeyote atakayeweza kufurahi akiona timu aliyofundisha kwa mafanikio makubwa inaanza kufanya hovyo kipindi anapoondoka na kuikabidhi kwa kocha mwingine.

“Kwanza ni lazima nihakikishe usajili tutakaofanya unaleta manufaa msimu ujao kwa kuiwezesha timu kufanya vyema kama ilivyokuwa msimu huu, pia kujiwekea mipango thabiti ya kutuwezesha kutimiza malengo yetu kimataifa,” alisema Pluijm.

Mholanzi huyo anatarajiwa kurejea nchini Jumatatu ijayo ili kuendelea na programu zake za kuinoa timu hiyo kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.

Yanga itaanza kampeni zake kwenye kundi A ugenini Juni 17, mwaka huu kabla ya kuvaana na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Juni 27, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumaliza mzunguko wa kwanza dhidi ya Medeama ya Ghana nyumbani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles