24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm aota kuivua ubingwa TP Mazembe

kocha-mkuu-wa-yanga-hans-van-der-pluijm-kushoto-kocha-msaidizi-juma-mwambusi-katikati-na-kocha-wa-makipa-juma-pondamali-katika-mechi-dhidi-ya-azam-jumamosi-17-10-2015_lolyn75ee56414w47jmhoccraNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amekamilisha programu mpya aliyoandaa kwa wachezaji wake kuhakikisha timu hiyo inatetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kufanya kweli katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwakani ili kuweka rekodi ya kuivua ubingwa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mikakati ya Pluijm ya kutaka kuivua ubingwa Mazembe, imewekwa wazi zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Tanzania Bara kufunguliwa.

Pluijm aliliambia MTANZANIA jana kuwa programu yake hiyo inawalenga wachezaji wake wote wakiwamo wapya watakaosajiliwa kipindi hiki cha dirisha dogo, huku akikwepa kuweka wazi nyota anaotaka kuwasajili.

Alisema programu hiyo imeandaliwa kwa ubora wa hali ya juu ili kuiwezesha Yanga kutetea ubingwa wake na kuongeza kasi ya kufikia mafanikio ya TP Mazembe ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Wachezaji walikua mapumzikoni baada ya ligi kusimama kwa muda, hivyo watakapoanza mazoezi leo nataka niandae kikosi bora chenye makali mara mbili zaidi ya ilivyokuwa awali katika mechi tisa tulizocheza,” alisema.

Pluijm ambaye kikosi chake hakijapoteza mechi hata moja tangu kuanza kwa Ligi Kuu, alisema kama programu yake itatendewa haki na kutimiza kila alichopanga malengo yake yatafanikiwa kwa asilimia kubwa na hakuna kitakachoshindikana.

Hata hivyo, katika mazoezi ya leo Pluijm atawakosa nyota wake walioitwa kuichezea timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi dhidi ya Algeria Jumamosi hii na kurudiana Jumanne wiki ijayo.

Ligi Kuu Bara ilisimamishwa kupisha maandalizi ya timu ya Taifa, Taifa Stars kuelekea mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Algeria Jumamosi hii, Yanga ilikuwa haijapoteza mchezo hata mmoja zaidi ya kupata sare mbili kati ya mechi tisa za ligi hiyo.

Hata hivyo, kikosi hicho cha Pluijm kipo nafasi ya pili nyuma ya vinara Azam ambao wao wamepata sare moja tu dhidi ya Wanajangwani hao.

Pluijm anatarajiwa kuanza maandalizi ya mzunguko wa pili leo katika Uwanja wa Polisi College, huku akiwasubiri nyota wake walio kwenye kikosi cha timu ya taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles