28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Pluijm aiponda BDF

yanga vs BDF IXNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM
KOCHA wa Yanga, Hans van Der Pluijm, amekasirishwa na mfumo wa kujilinda uliotumiwa na BDF XI kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Licha ya BDF kucheza kwa staili hiyo, Yanga ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Amissi Tambwe.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Pluijm alisema timu yake ilipata shida sana kucheza nyuma ya mabeki watano wa BDF na kupelekea kutumia mashambulizi ya pembeni ya uwanja.
“BDF ilijilinda sana kipindi cha kwanza na baada ya kuona hali inakuwa ngumu kucheza nyuma ya mabeki watano wa timu hiyo, tulibadilisha mfumo na kutumia mashambulizi ya pembeni ya uwanja yaliyotupatia mabao.
“Nimefurahishwa na ushindi huo lakini nilihitaji bao moja zaidi ili kujipa matumaini zaidi kwa mechi ya marudiano ugenini.
“Mechi ya pili tutacheza kwa tahadhari kubwa na nidhamu ya hali ya juu ili kulinda ushindi wetu na hatimaye kusonga mbele,” alisema.
Pluijm alisema uamuzi wake wa kumtoa Tambwe na kumuingiza Jerryson Tegete kipindi cha pili, ulikuwa ni wa kiufundi zaidi kwani mshambuliaji huyo alishindwa kushirikiana vema na Mrisho Ngassa aliyekuwa akiliandama kwa kasi lango la BDF.
Wakati Pluijm akieleza hayo, Kocha Mkuu wa BDF, Letang Kgengwenyane ‘Rasta’, alikisifia kikosi cha Yanga kwa kiwango bora walichokionyesha kwenye mchezo huo lakini akadai kuwa nao watashinda mchezo wa marudiano kama walivyoshinda wapinzani wao.
“Yanga ilicheza vizuri, wachezaji wake walizuia vizuri, walipasiana vizuri na kupiga faulo nzuri, pia nawapongeza vijana wangu kwa kucheza vema na kuhimili makali ya Yanga. Yanga ni bingwa dakika 90 za kwanza na sisi pia tutakuwa bingwa kwenye mechi ya nyumbani,” alisema.
Akizungumzia mchezaji wa Yanga aliyewapa shida, Letang alisema: “Aliyevalia jezi namba 17 (Ngassa) ni mchezaji hatari sana alitusumbua mno.”

Hata hivyo, Letang aliliambia MTANZANIA kuwa watajipanga vizuri kumzuia Ngassa kwenye mchezo ujao ili asilete madhara zaidi kama alivyofanya katika mechi iliyopita.
Mchezo wa marudiano unatarajiwa kufanyika jijini Gaborone, Botswana Februari 27, mwaka huu, ambapo Yanga inahitaji sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele.
Wakati huo huo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano yaYanga, Jerry Muro, aliliambia MTANZANIA jana kuwa timu hiyo itaondoka jijini Dar es Salaam leo kuelekea jijini Mbeya kwaajili ya mechi mbili za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City.

Yanga itashuka uwanjani Alhamisi hii kuvaana na Prisons kabla ya Jumapili kuvaana na Mbeya City.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles