27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda: Uamuzi wa madiwani Chadema umeshatolewa

Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Waziri Mkuu Mizengo Pinda

Na Debora Sanja, Dodoma

UAMUZI kuhusu hatma ya madiwani watatu wa Chadema katika Manispaa ya Ilemela waliofukuzwa na Meya wa Manispaa hiyo, Henry Mtata, umekwisha kutolewa.

Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akijibu swali la Mbunge wa Ilemelea, Highness Kiwia (Chadema) wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu.

Katika swali lake, Kiwia alitaka kujua lini madiwani watatu wa Manispaa ya Ilemela waliofukuzwa kwa madai ya kutohudhuria vikao vitatu watajua hatima yao.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu sasa ni miaka miwili wananchi wa kata tatu hawana wawakilishi na leo ni mara ya nne nauliza swali hili, sasa unawaambia nini wananchi wa kata hizo?” alihoji Kiwia.

Pinda alisema ni kweli suala la mgogoro wa madiwani hao limechelewa kushughulikiwa kutokana na kuwa la sheria zaidi.
“Kutokana na jambo hili kuwa la sheria, tuliunda jopo la wanasheria kufanya uchunguzi na kulishughulikia.
“Bahati wamemaliza kazi na walishalileta kwangu na juzi tu ndiyo nimesaini barua ya uamuzi kwenda Tamisemi (Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa),” alisema.

Katika swali la nyongeza Kiwia alitaka kujua kama uamuzi umeshatolewa na lini utawafikia wananchi na madiwani hao.

Pinda alisema anaamini Waziri wa Tamisemi hatachukua muda mrefu kupelekea uamuzi huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza uweze kuwafikia wahusika.

Madiwani waliofukuzwa ni Danny Kahungu wa Kata ya Kirumba, Abubakaar Kapela wa Kata ya Nyamanoro na Marietha Chenyege wa Kata ya Ilemela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles