33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

‘Photoshop’ ya JPM yamponza Idris, Makonda amuita polisi, Kigwangalla amtetea

Anna Potinus,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemtaka muigizaji wa vichekesho, Idris Sultan kufika katika kituo chochote cha polisi kilichopo karibu naye baada ya kufanyia ‘photoshop’ picha zake na kuweka kichwa cha Rais John Magufuli ikiwa ni sehemu ya vichekesho vyake.

Idris aliweka picha mbili katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram na kuambatanisha na ujumbe mfupi wa maneno uliosema “kwa siku moja tukabadilishana kazi ili aenjoy birthday yake kwa amani,” aliandika Idriss huku akilenga kumtakia heri Rais Magufuli katika siku yake hiyo ya kuzaliwa kwa njia ya utani.

Katika picha hizo, moja inamuonyesha Idris akiwa ameketi kwenye kiti cha Rais, Ikulu huku nyingine ikimwonyesha picha ya Rais Magufuli akiwa katika mwonekano wa msanii huyo.

Baada ya Makonda kuona picha hizo alimtaka msanii huyo kufika katika kituo cha polisi ambapo atakuta ujumbe ambao amemuachia akidai kuwa kitendo alichokifanya kinaonesha kuwa haijui mipaka yake ya kazi.

“Naona mipaka ya kazi yako hauijuwi, nenda sasa hivi kituo chochote cha polisi uwaambie Makonda kaniambia nije utakuta ujumbe wako,” ameandika Makonda katika ukurasa wake wa Instagram.

Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala ameonesha kushangazwa na kitendo cha msanii huyo kuitwa polisi kwa kusema kuwa Rais Magufuli ni mtu wa watu na kwamba Idriss anafahamika kuwa sanaa yake ni ya uchekeshaji.

“Nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi, akikamatwa mniambie, nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake! Wameonesha upendo,” ameandika Kigwangala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles