23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Phiri ajivunia chipukizi Simba

Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri
Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri

NA JUDITH PETER, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, amesema anajivunia kuwa na kikosi bora na imara chenye wachezaji chipukizi ambacho kinajiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara, itakayoanza Septemba 20, mwaka huu.

Katika msimu huu wa ligi, Simba imesajili wachezaji wengi chipukizi na kuwaondoa wakongwe baada ya timu hiyo kupata matokeo mabaya katika msimu uliopita na kumaliza ikiwa katika nafasi ya nne.

Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana, Phiri alisema kuwa kikosi cha Simba msimu huu kina tofauti kubwa ukilinganisha na kile alichowahi kukifundisha miaka ya nyuma, ambacho kilikuwa na wachezaji wengi wakongwe na wazoefu.

Alisema wachezaji hao chipukizi wamekuwa wakijituma katika mazoezi na wameonesha nidhamu ya hali ya juu tangu alipojiunga rasmi na Simba na amekuwa akifurahia kukifundisha kikosi hicho.

“Simba ya sasa ina tofauti kubwa sana na ile niliyowahi kuifundisha miaka ya nyuma, kwani uongozi umesajili wachezaji wengi chipukizi wenye uwezo, wanaojituma na wenye nidhamu ya hali ya juu ukilingalisha na ile iliyokuwa na wachezaji wengi wakongwe,” alisema Phiri.

Kocha huyo ambaye alijiunga na Simba ikiwa tayari imefanya usajili wa wachezaji, alisema kwa sasa hawezi kufikiria ni mchezaji gani anayemuhitaji kwa ajili ya kukiboresha kikosi chake, hivyo ana kazi kubwa ya kuhakikisha anatengeneza Simba imara yenye ushindani msimu huu.

Alisema ikiwa kuna mapungufu yatakayojitokeza katika mzunguko wa kwanza wa ligi, atalazimika kusubiri hadi dirisha dogo la usajili ili kuziba pengo litakalojitokeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles