Pele afanyiwa upasuaji wa figo

0
318

SAO PAULO, BRAZIL

MKONGWE wa soka nchini Brazil, Edson Arantes do Nascimento ‘Pele’, amefanikiwa kufanyiwa upasuaji wa figo katika hospitali ya Sao Paulo nchini humo baada ya kuugua kwa wiki mbili.

Mchezaji huyo wa zamani ambaye ameacha historia kubwa, alianza kuugua akiwa nchini Ufaransa wiki iliyopita na kukimbizwa hospitalini, kabla ya mwishoni mwa wiki iliopita kuruhusiwa kurudi nchini Brazil kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Hospitali ya Albert Einstein, wameweka wazi kuwa, kila kitu kimekwenda sawa na hali ya gwiji huyo wa soka inaendelea vizuri.

Kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni, staa huyo mwenye umri wa miaka 78, amekuwa akikimbizwa hospitalini mara kwa mara kutokana na tatizo hilo la figo pamoja na mkojo.

Katika historia yake ya soka, ameacha historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa Kombe la Dunia mara tatu akiwa na timu ya taifa ya Brazil. Hata hivyo, katika maisha yake ya soka alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 1,281 baada ya kucheza michezo 1,363 kwenye michuano mbalimbali. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here