22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Patrice Evra atundika daruga

Manchester, England

NYOTA wa zamani wa timu ya Manchester United, Patrice Evra, ametangaza kustaafu soka la kulipwa huku akiwa na umri wa miaka 38.

Beki huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa, alicheza soka la ushindani kwa kipindi cha miaka 20, huku akiwa amepita katika klabu nane na timu yake ya mwisho ilikuwa West Ham mwaka jana.

Kwa sasa mchezaji huyo anafikiria kutimiza ndoto zake za kuja kuwa kocha mwenye jina kubwa duniani kama alivyotabiriwa na kocha wake wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson. 

“Maisha yangu ya kucheza soka la kulipwa sasa rasmi yamefikia mwisho, kwa sasa nimeanza kufanya mafunzo ya ukocha kwa ngazi ya leseni B ya UEFA tangu mwaka 2013 na nataka kumalizia ili nikachukue leseni A ya UEFA.

“Kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu kama kila kitu kitakuwa sawa basi nitakuwa tayari kwa ajili kuchukua timu na kufundisha. Sir Alex Ferguson aliwahi kutabiri kuwa wachezaji hawa wawili Ryan Giggs na Patrice Evra watakuja kuwa makocha wenye ubora wa hali ya juu,” alisema mchezaji huyo.

Evra aliacha historia ndani ya klabu ya Manchester United huku akidaiwa kuwa miongoni mwa mabeki bora wa upande wa kushoto ndani ya Ligi Kuu England huku akicheza kwa miaka nane ndani ya Old Trafford.

Katika kipindi hicho akiwa na Manchester United, alicheza jumla ya michezo 379 kuanzia mwaka 2006 hadi 20014, kabla ya kujiunga na Juventus hadi mwaka 2017. Miongoni mwa historia aliyoiacha ndani ya Manchester United ni kutwaa mataji 15.

Klabu zingine ambazo mchezaji huyo alifanikiwa kuzitumikia ni pamoja na Marsala, Monza, Nice, Monaco, Marseille na West Ham United.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles