23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Papa Francis ziarani Japan

TOKYO, JAPAN

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis amewasili Japan anakotarajiwa kutoa risala kali ya amani dhidi ya nyuklia katika nchi pekee iliyowahi kuhujumiwa kwa mabomu ya atomiki.

Kiongozi huyo, mwenye umri wa miaka 82 anatekeleza dhamiri ya muda mrefu ya kuhubiri nchini Japan ambako miaka kadhaa iliyopita alitarajia angekuwa mmisionari.

Amewasili Tokyo na mvua kali na upepo, huku kofia yake nyeupe ikipeperushwa alipokuwa anateremka ngazi za ndege ya shirika la ndege la Thailand, akitokea Thailand.

Ziara yake ya siku nne itaanzia Nagasaki na Hiroshima, miji inayofungamanishwa daima na mabomu ya nyuklia yaliyodondoshwa mwishoni mwa vita vikuu vya pili vya dunia na kuangamiza maisha ya watu wasiopungua 74,000 Nagasaki na 140,000 Hiroshima. 

Katika miji yote hiyo miwili Papa Francis atazungumza na wahanga wa mashambulio ya mabomu ya atomiki. 

Papa Francis atahutubia mbele ya kumbusho la amani mjini Hiroshima-ushahidi wa shambulio la bomu la nyuklia lililodondoshwa  Agosti 6 mwaka 1945.

Katika ujumbe wake kwa wananchi wa Japan kupitia kanda ya video kabla hajaondoka Vatican, Papa Francis alikosoa vikali “matumizi mabaya ya silaha za nyuklia.”

“Pamoja nanyi, naomba Mungu silaha za maangamizi za nyuklia hazitotumika tena katika historia ya binadamu” alisema kiongozi huyo wa waumini bilioni 1.3.

Papa Francis amewasili Tokyo akitokea Thailand ambako alihubiri uvumilivu wa kidini na amani. 

Anatarajiwa kutoa nasaha kama hiyo nchini Japan yenye waumini 440,000 tu wa kikatoliki kutoka jumla ya wakazi milioni 126.

Jumatatu Papa Francis atakutana na wahanga wa majanga ya kimaumbile, “matetemeko ya ardhi,Tsunami na kuvuja mionzi ya nyuklia mwaka 2011” tukio lililoathiri sehemu kubwa ya kaskazini mashariki mwa Japan.

Amepangiwa pia kukutana na mfalme mpya Naruhito na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe pamoja na kuhutubia katika uwanja wa michezo mjini Tokyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles