Papa Francis atangaza vita unyanyasaji kijinsia

0
593
Papa Francis

VATICAN CITY,Vatican

KIONGOZI  wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amesema kwamba ukimya juu ya unyanyasaji wa kijinsia hauwezi  kuvumiliwa na ndio maana ameagiza uchunguzi ufanyike juu ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la  Washington, Theodore McCarrick, ambaye alijiuzulu mwezi Julai mwaka huu.

Kauli hiyo ya Papa ni  tamko rasmi  la Vatican ambalo limetangaza  kwamba Kanisa lilipaswa kukabiliana na  tatizo kubwa la  unyanyasaji kijinsia  ndani na nje ya chombo hicho cha imani.

Taarifa hiyo ya  Vatican iliyotolewa juzi ilieleza kwamba Papa Francis anafahamu na kusononeshwa na uchafu huo na shutuma zinavyosababisha aibu kwa watumishi wa kanisa hilo.

“Vikwazo vyote na mizizi yake  haviwezi tena kuvumiliwa  na  Kanisa lilikuwa na wajibu kuzuia uhalifu huo usiojitokeza katika siku zijazo kwa watu wasiokuwa na hatia zaidi na walioathirika zaidi katika jamii,”ilieleza taarifa ya  kiongozi huyo.

Taarifa hiyo pia imesisitiza kwamba pia Papa Francis  katika barua ya ujumbe ambao aliutuma Agosti kwa wakatoliki wote alieleza kwamba njia pekee ambayo tunapaswa kuitumia kukomesha uovu huu   huu ambao umesitisha maisha ya wengi sana ni kutambua kuwa sisi sote ni watoto wa Mungu.

“Uelewa huu ukiwa  sehemu ya watu na historia iliyoshirikishwa itatusaidia kutambua dhambi na makosa yetu ya zamani kwa uwazi wa uhalifu ambao unaweza kutuwezesha kusavishika upya ndani ya nafsi zetu,” alieleza  taarifa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here