Imechapishwa: Fri, Apr 13th, 2018

PAPA FRANCIS AKIRI ALIFANYA MAKOSA CHILE

VATICAN CITY, VATICAN


KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amekiri kufanya makosa makubwa katika maamuzi aliyoyachukua kuhusu sakata la udhalilishaji wa ngono nchini Chile.

Kwa sababu hiyo amewaalika waathirika wa vitendo hivyo mjini Rome ili kuwaomba radhi.

Katika barua ya umma isiyo ya kawaida, Papa Francis pia amewataka maaskofu wote wa Chile kufika Makao Makuu ya Kanisa, Vatican kwa mkutano wa dharura utakaofanyika wiki chache zijazo.

Mkutano huo unatarajia kujadili namna ya kurekebisha maafa yaliyotokana na kashfa hiyo ambayo imeichafua taswira ya Kanisa Katolini nchini Chile na sifa ya Papa.

Papa Francis amelaumu ukosefu wa taarifa sahihi na zenye urari wakati wa kumtetea Askofu Juan Barros alipofanya ziara nchini Chile Januari mwaka huu.

Barros alishutumiwa na waathirika wa kashfa hiyo kuwa alishudia na kuupuza madhila dhidi yao wakati Padri Fernando Karadima alipowadhalilisha kingono.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

PAPA FRANCIS AKIRI ALIFANYA MAKOSA CHILE