30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Papa Francis aingilia kati mzozo Venezuela

Pope Francis Holds His Weekly General AudienceCARACAS, VENEZUELA

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amechukua hatua isiyotarajiwa na kuingilia kati kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa nchini Venezuela.

Taifa hilo pia linakabiliwa na matatizo ya kiuchumi.

Wakati wa mkutano wa faraghani na Rais Nicolas Maduro uliofanyika Vatican, Papa Francis aliomba kuongoza mashauriano kati ya rais huyo na viongozi wa upinzani.

Awali Papa Francis alimshauri Rais Maduro kufuata njia ya mazungumzo ya uaminifu na yenye kuleta tija, ili kupunguza matatizo yanayowasibu watu wa Venezuela.

Mjumbe wa Papa nchini Venezuela, Emil Paul Tscherrig amesema pande zote mbili zimeahidi kufanya majadiliano rasmi Jumapili ijayo katika kisiwa cha Margarita, Venezuela.

Lakini kupitia taarifa iliyorushwa mtandaoni, Kiongozi wa Upinzani Henrique Capriles amesema hakuna mazungumzo yoyote yaliyoanza na kwamba tangazo la kuanza upya kwa mashauriano ni njama ya serikali kupoteza malengo.

Wasiwasi umekuwa ukitanda nchini Venezuela kutokana na kuahirishwa kwa kampeni za kura ya maoni ya kuamua kuhusu kuondolewa madarakani kwa Rais Maduro.

Upinzani katika taifa hilo la Amerika Kusini linalozalisha mafuta kwa wingi, unaendesha kampeni hiyo ya kutaka kumuondoa Rais Maduro, ukimlaumu kwa mgogoro huo wa kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles