23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

PANYA WAATHIRI HEKA 100,000 ZA MPUNGA, MAHINDI

Na ASHURA KAZINJA-MOROGORO



ZAIDI ya ekari 140,000 za mazao ya mahindi, mpunga na mihogo zimeathiriwa na panya, kuanzia Julai mwaka jana mpaka mwanzoni mwa mwaka huu katika halmashauri 21 nchini.

Akizungumza na MTANZANIA jana kwenye kituo cha kudhibiti baa la Panya kilicho chini ya Wizara ya Kilimo, Ofisa Kilimo, Christina Tewele alisema uvamizi wa Panya katika wilaya hizo unatishia upatikanaji wa uhakika wa chakula kwa msimu ujao wa mavuno

Alisema jitihada zilizofanywa na kituo hicho kupitia Wizara ya Kilimo na Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo ni pamoja na kupeleka sumu aina ya Zinc, zaidi ya tani 800 kwa ajili ya kudhibiti panya waharibifu wa mazai katika halmashauri za wilaya 12 kati ya 21 zilizokumbwa na tatizo hilo.

“Kuna ekari zilizoathiriwa na Panya ambazo ni zaidi ya 140,000, hata hivyo jitihada zinaendelea kufanywa kuhakikisha wanadhibitiwa ili kuwasaidia wakulima wasipate hasara na kukosa mavuno ya kutosha kwa msimu huu.

“Tatizo linasababishwa na baadhi ya wakulima kutosafisha mashamba yao vizuri kwa sababu inatakiwa pembezoni mwa shamba kusiwe na vichaka, mita 100 kutoka mwisho wa shamba ili wakulima katika kutambua eneo lao limevamiwa na panya ni mpaka wafike idadi ya 700 hadi 1000,” alisema Tewele.
Mtengenezaji wa Mitego ya Panya Mjini Morogoro, Idd Chilongola alisema aliamua kubuni mitego ya Panya baada ya kusikia taarifa kuwa wameibuka.

Aliema mtego mkubwa anauuza Sh 35,000 ambao una uwezo wa kukamata panya zaidi ya 50 kwa wakati mmoja baada ya kuweka chambo zikiwemo pumba.
“Wakulima watumie mitego rahisi ambayo ni ya kununua ndoo za lita kumi, idadi kulingana na ukubwa wa shamba, chimbia chini kisha jaza maji, pembeni weka pumba kama chambo ili wakija kula watumbukie majini,” alisema Chilongola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles