31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

PANYA, MENDE WASHAMIRI IKULU YA MAREKANI

JOSEPH HIZA NA MASHIRIKA 

RAIS Donald Trump anayefahamika kwa ubilionea, ufahari, majivuno aliwahi kukana kutamka hilo, lakini ushahidi sasa umefichuka kuwa hali ya Ikulu ya Marekani maarufu kama White House ilistahili kile alichokana kukitamka.

Mapema wiki hii utata uliibuka wakati Jarida la Golf Magazine lilimtuhumu Trump akisema: “White House ni jalala kweli kweli.’

Mara moja akifahamika jumba hilo kuwa kipenzi namba moja kwa Wamarekani, Trump anayejidai kuwa mzalendo namba moja, ndiyo maana kaja na sera ya Marekani Kwanza alikanusha kutoa matamshi hayo na suala hilo likatawala siasa.

Lakini kauli hiyo aliyoikana kuitoa inafanana na kile wafanyakazi wa kampuni zilizopewa kazi za kufanya ukarabati na marekebisho katika maeneo mbalimbali ya Ikulu ya Marekani maarufu kama Whitehouse walichokiona.

Ni kutokana na wingi wa panya, mende na wadudu wengine wadogo wadogo waliotawala katika majengo ya makazi hayo makongwe nchini humo.

Licha ya ukongwe wake kutokana na heshima palipojijengea kwa kuishi mtu mwenye nguvu kuliko wote nchini humo na duniani kwa ujumla, haikutarajiwa kukutana na wadudu hao wanaoshamiri maeneo machafu.

Hayo yamebainika kufuatia kutolewa kwa ripoti ya vitu vinavyopaswa kurekebishwa katika makazi hayo, ambayo kwa sasa yanamilikiwa na Rais Donald Trump.

Ikulu ya White house, ambayo chombo cha habari cha NBC Washington kiliiona na kushirikisha ripoti nyingine ya mwaka uliopita ya wakati wa utawala wa Rais Barack Obama.

Panya, mende, wadudu na vyoo vilivyovunjika au kuchakaa ni miongoni mwa vitu vingi vilivyoripotiwa zaidi kwa wafanyakazi wa kufanyia marekebisho na kuipamba Whitehouse.

Panya wanadaiwa kuonekana katika majengo mbalimbali ikiwamo chumba cha kulia chakula cha maafisa wa jeshi la wanamaji kwa mujibu wa Brian Miller, Inspekta Jenerali wa kikosi cha huduma za jumla ambacho husimamia marekebisho katika makazi hayo ya rais.

”Mtu yeyote kati yetu ambaye anamiliki nyumba ya zamani anajua kwamba inahitaji kazi nyingi, lakini ni ajabu kukutwa kwa makazi haya ambayo yalipaswa kuwa safi.

Mende walikuwa tatizo katika chumba cha kulia chakula huku wadudu wengine wadogo wakionekana katika nyumba anayoishi afisa mkuu wa jeshi kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Wadudu na mende pia walionekana katika chumba cha wanahabari huku panya na sisimizi wakionekana kwa wingi katika ofisi ya mnadhimu mkuu wa Whitehouse

Mbali na kukabiliana na wadudu ,ripoti hiyo ya marekebisho ya Ikulu inaonyesha kazi nyingi zilizohitajika kufanyika baada ya utawala mpya kuingia mwanzoni mwa mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles