PAMBA YAJIPANGA KUREJEA LIGI KUU

0
1008

Na MASYENENE DAMIAN, MWANZA

TIMU ya Pamba ya Mwanza imeanza maandalizi kujiandaa na Ligi

Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) itakayoanza Septemba 20.

Pamba imepangwa kundi B pamoja na timu za Arusha FC na Arusha United zote za mkoani Arusha, Boma Mbeya,

Dodoma FC, Geita Gold Sports, Green Warriors na Transit Camp za Dar es

Salaam, Mashujaa ya Kigoma, Mgambo Shooting na Rhino Rangers za

Tabora na Polisi Tanzania kutoka Kilimanjaro.

Awali timu hiyo ilimtangaza Kocha Hassan Banyai kuwa Kocha Mkuu,

akichukua nafasi ya Venance Kazungu, lakini ilishindikana baada ya kushindwa kufikiana makubaliano, sasa timu hiyo itafundishwa na Juma Yusuph.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Johnson James, alisema kikosi chao chenye wachezaji 30

waliosajiliwa msimu huu kimeanza kambi na kinafanya mazoezi yake

katika Uwanja wa Airpot Ilemela.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here