P-SQUARE WAPIGA BEI MJENGO WAO

0
48

LAGOS, NIGERIA

NYOTA wa muziki nchini Nigeria waliokuwa wanaunda Kundi la P-Square, Peter na Paul Okoye, wametangaza kuuza nyumba yao iliyopo jijini Lagos.

Hatua hiyo imefikia mara baada ya kundi hilo kuvunjika kutokana na migogoro na kifamilia, huku Peter akidai kaka yao Jude Okoye alimtishia maisha na mke wake, hivyo hawawezi kuwa karibu tena hata kama ni familia moja.

“Naomba niweke wazi kuwa P-Square haipo tena na haiwezekani, kila mmoja anafanya yake sasa hata kama Paul anaandika kwenye kurasa zake za Instagram kwamba damu ni mzito kuliko maji, sasa nani damu na nani maji?

“Kila mtu anatakiwa kuishi na mambo yake, ndiyo maana ni bora kuuuza nyumba yetu, kila mtu afe na chake,” alisema Peter.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here