33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Oxygen yatoa msaada wa mitungi ya gesi Hospitali ya Bombo

Amina Omari, Tanga

Hospitali ya Rufaa ya Bombo mkoani Tanga imepokea msaada wa mitungi 50 ya gesi kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wenye tatizo la kupumua.

Msaada huo uliotolewa na kampuni ya oxygen product E .A Company LTD imepokelewa na Mkuu wa mkoa huo, Martin Shigela.

Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Mohamed Abnoor amesema wana lengo la kusaidia wagonjwa wenye uhitaji watakaofikishwa katika  hospitali hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mganga mkuu wa mkoa, Dk. Naima Yusuph amesema hospitali hiyo ilikuwa na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo hivyo msaada huo umekuja wakati muafaka.

“Sasa wagonjwa 100 wataweza kupatiwa huduma ya oxygen kwa wakati mmoja kwani mtungi mmoja una uwezo wa kuhudumia wagonjwa wawili, “amesema Dk. Yusuph.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles