24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa tishio

Mwandishi Wetu- Tabora

IDARA ya Afya mkoani Tabora, imesema  jitihada za makusudi zinahitajika kuzuia na kudhibiti ongezeko  kubwa la magonjwa yasiyoambukiza mkaoni humo.

Baadhi ya magonjwa yasiyoambukizwa ni kisukari, shinikizo la damu, seli mundu, saratani , magonjwa ya akili na pumu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni wa kuzuia na kudhibiti magonjwa hayo, Katibu Tawala Msaidizi (Afya), Dk. Honoratha Rutatinisibwa alisema tangu mwaka 2017 hadi mwaka huu, kumekuwapo na ongezeko la magonjwa hayo mkoani humo.

Alitaja baadhi ya wagonjwa yasioambukizwa yaliongezeka na idadi kwenye mabano, ni ni kisukari ambapo mwaka 2017 (4,345) na kuongezaka  hadi (6,732), mwaka huu ikiwa ni ongezeko la wagonjwa (2,387) sawa na asilimia 35.

Alisema ugonjwa wa shikizo la damu, wagonjwa wameongezeka katika kipindi hicho kutoka 13,940 hadi 9,460, ikiwa ni ongezeko wagonjwa 5,520 sawa na asilimia 28.

Alisema ugonjwa wa pumu, umeongezeka kutoka wagonjwa 5,338 hadi 8,434, ikiwa kuna ongezeko la wagonjwa 3,096 sawa na asilimia 37 ndani ya kipindi hicho hicho.

Akizungumza wakati wa kilele cha wiki ya maadhimisho ya kupambana na magonjwa hayo ,Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Komanya Kitwala aliwataka wakazi wa mko huo kujenga tabia ya kuchunguza afya zao  mapema walau mara mbili kwa mwaka.

Alisema hatua hiyo itasaidia kugundua matatizo mapema na kuwahi kukabiliana nalo likiwa bado katika hatua za awali kwa kutumia  gharama kidogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles