26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

OMMY DIMPOZ KUWASHANGAZA  MASHABIKI WAKE

Na JENNIFER ULLEMBO


MSANII wa muziki wa kizazi kipya,  Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, amesema anajipanga kufanya kitu kitakachowashangaza  mashabiki na wadau wa muziki nchini.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ommy Dimpoz alisema hawezi kuzungumza sana kitu alichokiandaa kukifanya hivyo mashabiki wasubiri.

“Ninajipanga kuwashangaza mashabiki zangu, wajiandae  kusikia kile nitakachokifanya, nimekuwa nikisafiri mara kwa mara wakati huu ambao nipo kimya, nimefanikiwa kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vimefumbua akili yangu,” alisema Dimpoz.

Alisema mashabiki wamekuwa wakilalamika na kudai amefulia, jambo ambalo halina ukweli wowote kwani kila kitu kinafanyika kwa mipango.

Alisema kuwa kimya kwa muda mrefu si sababu ya kufulia au kushindwa kuendelea na fani kama ambavyo mashabiki wengi wamekuwa wakisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles