31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Olunga mashakani kutua Simba

40FBFEF7E486A9775FA2A703837AF071*Gor Mahia wataja dau kubwa, Kerr asema hajaona alichofanya Chalenji

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

MPANGO wa klabu ya Simba kumnasa Straika wa Gor Mahia, Michael Olunga, umeingia mushkeli baada ya klabu yake kuitaka Simba ilipe dola 200,000 (zaidi ya Sh milioni 400 za Tanzania), kitu ambacho ni kigumu kwa klabu ya Wekundu hao wa Msimbazi kulipa kwa sasa.

Simba ilianza kumfukuzia Olunga tangu kwenye michuano ya Kagame, iliyofanyika hapa nchini kwa Azam kuwa mabingwa, lakini walishindwa kuafikiana na timu hiyo.

Habari za ndani ilizozipata MTANZANIA, zimedai kuwa dau hilo la Gor Mahia limeonekana kuwa ni kubwa sana kwa Simba, hivyo kuanza kupoteza matumaini ya kufanikisha mpango wao huo.

“Hela hiyo ni nyingi sana na inaweza kutumika kusajili wachezaji wengi zaidi, hivyo kwa sasa uhakika wa kumpata tena Olunga ni mdogo, labda hadi atakapomaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi huu, ambapo tunaweza kufanya naye mazungumzo kama mchezaji huru na kumsajili kwa ajili ya kumtumia msimu ujao,” kilisema chanzo cha habari hizi.

Chanzo hicho ambacho hakikutaka kutajwa jina lake gazetini kilieleza kwa upande wa mchezaji Paul Kiongera, yeye atajiunga na wenzake hivi karibuni kama walivyokuwa wametangaza awali, kumalizia mkataba wake wa miezi saba uliobaki na baadaye kuangalia kama wanaweza kufanya mazungumzo naye kwa ajili ya kuongeza mkataba.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Dylan Kerr, amedai kuwa hakuna alichokifanya Olunga kwenye michuano ya Chalenji akiwa na timu yake ya Kenya, ambao wametolewa hatua ya robo fainali huku akidai kutokumfahamu Kiongera.

“Sijui walichokifanya kwenye timu zao za huko Kenya, lakini Olunga sijaona alichokifanya kwenye michuano ya Cecafa Ethiopia.

“Hivi Ligi Kuu ya Kenya ni bora kuliko ya Tanzania? Wachezaji wake ni wazuri kuliko wa huku? Kwanini wanawachukua?” alihoji Kocha huyo.

Awali Kerr kabla ya kuanza kwa usajili huu mdogo alipanga kuongeza wachezaji, hasa wa ndani, ili kuweza kukipa nguvu kikosi chake huku akiamini kuwa Tanzania ina wachezaji wengi wazuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles