23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

OKWI, MAKAMBO WAWASHTUE WACHEZAJI WAZAWA

 MWANDIDHI WETU -DAR ES SALAAM 

KIU ya mashabiki, wanachama na wapenzi wa Simba ni kumuona straika wao wa zamani, Emmanuel Okwi akivaa tena jezi lenye rangi nyekundu au nyeupe ambayo imekuwa ikitumiwa na klabu hiyo. 

Hilo ni kwa upande wa Simba, lakini kwa upande wa mashabiki, wanachama na wapenzi wa vigogo wengine wa soka la Tanzania, timu ya Yanga, shauku yao ni kumuona kwa mara nyingine mshambuliaji wao wa Zamani Heritier Makambo akiwatumikia msimu ujao. 

Wachezaji hawa wawili walionekana kukata kiu za wadau wa klabu hizo pamoja na viongozi wao kutokana na kiwango bora walichokionyesha wakati wanazitumikia timu hizo. 

Nianze na Okwi aliondoka Simba msimu uliopita baada ya mkataba wake kumalizika na kupata dili la kujiunga na Al Ittihad ya Mirsi iliyomuona wakati wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika(AFCON). 

Mchezaji raia wa Uganda, aliondoka kipindi ambacho alikuwa bado anahitajika Msimbazi, hivyo ikawalazimu Wekundu hao kumsajili Mbrazil Wilker da Silva ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji. 

Hata hivyo, Silva alishindwa kuonyesha makali yaliyotarajiwa. 

Okwi ni mchezaji aliyekuwa na msaada mkubwa wakati Simba ilipotinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo kuondoka kwake ikawa ni pengo. 

Imekuwa ni kawaida kwa nyota huyo, Mganda kuondoka Simba na kurejea tena, ameshafanya hivyo mara tatu. 

Kingine kinachoonekana kuongeza uzito wa Okwi kuhitajika kurejea katika timu hiyo, ni maandalizi ya Simba kuelekea kwenye mchiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa sababu nafasi ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara ni kubwa. 

Ikumbukwe Okwi alijiunga na Simba kwa mara ya kwanza mwaka 2010 aki

 tokea SC Villa ya Uganda, akacheza hadi 2013, akauzwa kwenda Étoile du Sahel ya Tunisia.

Hata hivyo alikaa kwa muda mfupi katika timu hiyo ambayo iliamua kumtoa kwa mkopo Villa lakini hakudumu baada ya kurejea Tanzania kujiunga na Yanga katika msimu wa 2013/2014

Alicheza Yanga kwa muda mfupi, kisha kurejea Simba, akacheza mwaka mmoja, baadaye akasajiliwa na Sonderjyske ya Denmark aliyocheza kuanzia 2015-2017.

Baada ya kumaliza mkataba, Okwi alimua kurudi tena katika timu yake ya zamani, Villa lakini hakudumu akarudi Simba msimu wa 2017/2018.

Na katika kipindi hiki, tayari ana husishwa na kutakiwa kurejeshwa Msimbazi, kwakua mabosi wa klabu hiyo hawajaridhishwa na viwango vya wale waliosajiliwa ili kuziba pengo lake.

Uongozi wa Simbam kupitia kwa Ofisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mbatha, umeweka wazi kuwa hautasita kumrejesha Okwi katika kikosi chao ikiwa kocha wao, Sven Vandenbloeck atawasilisha ombi hilo.

Senzo amekaririwa akisema, Okwi ni mchezaji mzuri na rekodi yake inafahamika katika klabu yao hiyo.

Kwa Makambo, naye baada ya kuichezea Yanga kwa msimu mmoja, aliuzwa kwenda katika klabu ya Horoya FC ya Guinea.

Hata hivyo, huko mambo yameonekana kuwa magumu kwake kwani hajafanikiwa kuingia katika kikosi cha wachezaji 11 wa kwanza, badala yake amekuwa akianzia benchi.

Licha ya hayo yote yanayomkumba Makambo raia wa DRC, bado anaonekana kuwa lulu Jangwani.

Wadau wa Yanga wanaamini safu yao ya ushambuliaji imepoa licha ya usajili wa wachezaji kadhaa uliofanywa baada ya kuondoka kwa Makambo.

Hii ina maana gani, lipo la kujifunza hapa hasa kwa wachezaji wetu wazawa wanaozichezea timu hizi mbili, nalo ni kuboresha viwango zaidi ili kutoa mchango utakaowafanya Okwi na Makambo kusahaulika.

Hatua ya viongozi wa timu hizo kufikiria kuwarejesha Okwi na Makambo kinapaswa kuwasonesha wachezaji wazawa wa timu hizo na kujiona wana deni kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles