29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

OBAMA, PUTIN WAMLILIA  ANNAN

ACCRA, Ghana


VIONGOZI wa mataifa mbalimbali na Jumuiya za Kimataifa wameomboleza kifo cha Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa,(UN)  na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel,  Kofi Annan  aliyefariki dunia juzi akiwa na umri wa miaka  80.

Miongoni mwa viongozi   waliotuma   salamu za rambirambi kwa familia na viongozi wa nchi hii, ni Katibu Mkuu wa sasa wa  UN, Antonio Guterres,  Rais wa Urusi,  Vladimir Putin  na Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, ambao walimuelezea Annan kama alikuwa kiongozi wa kuigwa na aliyesimamia vema dunia.

Annan,   raia Ghana, aliitumikia UN kuanzia mwaka 1997 hadi  2006  na ndiye mwafirika wa kwanza kushika wadhifa huo katika taasisi hiyo kubwa duniani.

Baada ya kipindi hicho  hadi anafariki dunia ndiye aliyekuwa msuluhishi katika mgogoro wa Syria akiongoza jitihada za kumaliza mfarakano uliopo nchini humo.

Mwanadipolomasia huyo alifariki dunia  juzi katika hospitali  mjini  Bern,   Uswisi   baada ya kuishi nchini humo kwa   miaka saba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi yake, kiongozi huyo alifariki dunia  Jumamosi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais Putin alisema   kumbukumbu ya Annan itaendelea kudumu mioyoni mwa  wananchi wake.

Kwa upande wake Obama, ambaye pia   ni mwafrika wa kwanza kuingia Ikulu ya Marekani, alisema   baada ya kuvuka vikwazo vyote Annan hakuacha kusimamia jukumu  la kuhamasisha kuwapo  dunia  yenye amani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles