31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Obama amkosoa Trump jinsi ya kukabili corona

WASHINGTON, Marekani

RAIS mstaafu wa Marekani, Barrack Obama kwa mara nyingine tena amemkosoa mrithi wake, Donald Trump kwa jinsi anavyolishughulikia suala la virusi vya ugonjwa wa corona.

Katika hotuba kwa hafla iliyorushwa  kupitia mtandao, alisema  mlipuko wa virusi vya corona umedhihirisha maofisa wengine hawafanyi kazi walioajiriwa kusimamia.

Alisema ni ‘janga la machafuko’ jinsi Rais Trump anavyoangazia suala hilo katika mkutano uliovuja wiki iliopita.

Obama aliwahutubia wanafunzi wa shule katika sherehe ilioandaliwa na LeBron James na ilikuwa mojawapo ya programu maalumu ambayo ilishirikisha watu maarufu kama vile ndugu wa Jonas, Megan Rapinoe, Pharrell Williams na mwanaharakati wa elimu, Malala Yousafzai.

Katika hotuba yake kwa takriban zaidi ya taasisi 10 za wanafunzi weusi na vyuo vikuu, Obama alisema Covid-19 ilifichua mianya na makosa katika uongozi wa taifa hilo.

”Zaidi ya chochote kile janga hili linaonesha wazi  wengi wa maofisa walio uongozini hawajui wanachofanya”, alisema.

Zaidi ya watu 1,200 wamefariki kutokana na virusi vya corona nchini Marekani katika kipindi cha saa 24, kulingana na takwimu mpya kutoka Chuo Kikuu cha John Hopkins.

Idadi ya watu waliofariki ni 89,000, ambayo ndio ya juu zaidi duniani.

Obama pia alizungumzia kwa urefu jinsi virusi hivyo vinavyozidi kuiathiri jamii ya watu weusi nchini humo.

”Ugonjwa kama huu unafichua ukosefu wa usawa uliopo na mzigo wa ziada ambao jamii ya watu weusi wamekuwa wakikabiliana nao katika historia ya taifa hili”, alisema.

Idadi kubwa ya Wamarekani weusi, wamekufa na wengine kulazwa hospitalini.

Rais huyo wa zamani pia alizungumzia kuhusu mauaji ya Ahmaud Arbery aliyekuwa akifanya mazoezi ya kukimbia  ambaye alipigwa risasi na maofisa wa polisi weupe Februari, mwaka huu – katika hotuba yake.

Alisema  ubaguzi wa rangi ulibainika wazi nchini humo wakati mtu mweusi anapofanya mazoezi ya kukimbia na watu fulani wanahisi wanaweza kumsimamisha na kumuuliza maswali na kumpiga risasi, anapokataa kuwajibu.

”Iwapo dunia itaimarika , itategemea nyinyi”, aliwaambia mahafala hao.

Obama amenyamaza kwa kipindi kirefu tangu alipoondoka madarakani mnamo Januari, 2017 na hajawahi kuzungumzia kuhusu vitendo vya mrithi wake.

Lakini wawili hao, wamekabiliana vilivyo katika siku za hivi karibuni, hatua iliomfanya Rais Trump kumshutumu Obama na washauri wake kwa kuendeleza juhudi za kihalifu kuhujumu utawala wale.

”Ni uhalifu mkuu wa kisiasa katika historia ya Marekani , kwa kiwango kikubwa”, rais huyo aliandika katika mtandao wake wa twitter wiki iliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles