25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Nzige wa jangwani wavamia Uganda

Kampala, Uganda

Uganda imethibitisha uvamizi wa nzige wa jangwani katika eneo la Karamoja lililo mashariki mwa nchi hiyo.

Kundi la kwanza la nzige lilionekana saa tisa mchana siku ya Jumapili katika wilaya ya Moroto.

Makundi mawili ya wadudu hao waharibifu yamegunduliwa eneo la Karamoja nchini Uganda.

Serikali ikishirikisha majeshi imewapeleka makundi ya maofisa na wataalamu kupambana na nzige hao.

Katika muda wa saa tatu tu baada ya nzige hao kuonekana mpakani, walikuwa wamefika katika wilaya mbili jirani za Amudat na Nakapiripirit.

Kundi hilo la nzige linadhaniwa lilitokea eneo la Pokot Magharibi nchini Kenya.

Kwa kuwa nzige hao wanasambaa kwa kasi kubwa, maafisa wa wizara ya kilimo wanasema watalazimika kusambaza vifaa maeneo mbalimbali ili kukabiliana nao.

Baadhi ya nchi za Afrika ambazo zimeathiriwa na uvamizi wa nzige hao ni Kenya, Somalia na Ethiopia

Mara tu baada ya taarifa za nzige hao kuthibitishwa, makundi ya maofisa na majeshi wamelekwa katika maeneo yaliyovamiwa kwa lengo la kuwanyunyuzia dawa kama hatua ya kwanza kukabiliana nao.

Waziri mkuu Dk. Ruhakana Rugunda ametoa wito kwa wananchi wote kushiriki katika zoezi la kukabiliana na nzige hao ambao wameelezewa kuwa wataathiri upatikanaji wa chakula na uchumi kuanzia ngazi ya familia.

Wizara ya kilimo imefafanua kuwa imekuwa ikijiandaa kukabiliana na uvamizi wa nzige hao kwa muda wa wiki mbili sasa tangu ilipobainika kwamba walikuwa kilomita chache kutoka mpaka wa Uganda na Kenya.

Nzige wa jangwani ni waharibifu kwa mimea na mavuno ya shambani

Huku akisisitiza kuwa kemikali zinazotumiwa kuangamiza nzige hao hazina madhara kwa binadamu, Kamishna wa Idara ya Kulinda Mimea, Stephen Tibaijuka amelezea kuwa vifaa vyote vinavyohitajika vilikwisha wasilishwa eneo la Karamoja.

Kulingana na shirika la chakula na kilimo duniani uvamizi huu wa nzige ndiyo mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 70.

Kundi moja la nzige laweza kuharibu chakula cha hadi watu 2,500 kwa siku moja tu, na hujumuisha wadudu milioni 150 katika eneo la kilomia moja mraba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles