28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Nyumba za Mchungaji Lwakatare zavunjwa

Mchungaji wa Kanisa la Assemblies Of God Mikocheni, Dk. Getrude Lwakatare
Mchungaji wa Kanisa la Assemblies Of God Mikocheni, Dk. Getrude Lwakatare

MANENO SELANYIKA NA VICTOR MRUTU (TUDARCO)

SERIKALI jana imebomoa nyumba nne za Mchungaji wa Kanisa la Assemblies Of God Mikocheni, Dk. Getrude Lwakatare, zilizopo Mtaa wa Palm Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa Mchungaji Lwakatare alikuwa anamiliki eneo hilo kinyume na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Baraka Mkuya, alisema uamuzi huo umetoka ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Manispaa ya Kinondoni.

Alisema nyumba hizo, zimevunjwa kwa kuwa zimejengwa bila kibali cha ujenzi kutoka Manispaa ya Kinondoni.

“Mama Lwakatare hana hati ya kumiliki eneo hili wala kibali cha kujenga nyumba kutoka Manispaa ya Kinondoni.

“Wizara imetambua nyumba hizi zimejengwa eneo ambalo si sahihi, ndiyo  maana manispaa imeagiza zibomolewe,” alisema Mkuya.

Alisema manispaa ndiyo yenye uwezo wa kutoa kibali cha ujenzi wa eneo hilo na si chombo kingine.

Awali ofisi ya Ardhi ilipokea malalamiko kutoka kwa mmiliki halali wa eneo hilo, Janeth Kiwia, kwamba eneo lake limevamiwa na kujengwa bila kibali Desemba 24, mwaka jana.

Baada ya kupata taarifa hiyo, wizara ilifanya uchunguzi na kubaini ukweli wa umiliki wa eneo hilo, na ikaamua kusimamisha shughuli zote.

Mmiliki halali wa eneo hilo, Kiwia, alisema analimiliki muda mrefu kwa jina la shemeji yake ambaye kwa sasa ni marehemu.

Alisema baada ya shemeji yake kufariki dunia mwaka 2010, ndipo alipofuata utaratibu wa kisheria na kusajili jina lake.

“Nikiwa nje ya nchi, nilipata taarifa mama Lwakatare na wanae wamevamia eneo langu lililokuwa na vyumba vinne vya kulala, nilikuwa ninaendelea kujenga kidogo kidogo kutokana na uwezo wangu mdogo.

“Mama mchungaji nilipata taarifa alikuwa akijisifu kwamba yeye ni mbunge hawezi kushindwa na raia.

“Hivyo aliwaambia mafundi wake waendelee na ujenzi ambapo walikuwa wakijenga usiku na mchana,” alisema Kiwia.

Hata hivyo, Mwanasheria wa Lwakatare, Emmanuel Augustino, alisema uamuzi wa kubomoa jengo hilo haukufuata sheria kwa sababu suala hilo lipo mahakamani.

Alisema kesi itasikilizwa tena Agosti 20, mwaka huu katika Baraza la Ardhi la Manispaa ya Kinondoni.

Kwamba kutokana na hali hiyo, atashauriana na mteja wake ili waweze kufungua kesi ya madai.

Alisema nyumba hizo zina thamani ya zaidi ya Sh. milioni 800.

Baadhi ya majirani waliozungumza na MTANZANIA, walisema walikuwa wakimuona Mchungaji Lwakatare akitembelea eneo hilo nyakati za usiku.

Walisema ujenzi huo, ulikuwa ukiendelea kwa kasi mno usiku na mchana tofauti na maeneo mengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles