NYUMBA YA WIZ KHALIFA YAVAMIWA

0
449

 

Los Angeles, Marekani


STAA aliyetamba na wimbo wa ‘See You A Gain’, Cameron Thomaz maarufu kwa jina la Wiz Khalifa, ameripotiwa kuwa nyumba yake ya jijini Los Angeles nchini Marekani, juzi ilivamiwa na majambazi, lakini hakuna kitu kilichoibiwa.

Inadaiwa kwamba, ilikuwa saa 10:45 usiku majambazi walivamia nyumba hiyo baada ya kuvunja dirisha, lakini hawakuondoka na kitu chochote.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, wakati tukio hilo linatokea, msanii huyo alikuwa kwenye ziara ya muziki jijini Texas.

Tukio hilo linadaiwa kuwa la tatu jijini Los Angeles upande wa mastaa ndani ya mwezi mmoja, staa wa muziki na filamu, Bella Thorne, Jumanne jioni wiki iliyopita nyumba yake ilivamiwa, huku John Mayer akiwa wa kwanza mwezi huu nyumba yake kuvamiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here