24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Nyota ya Dk. Mwele yazidi kung’aa kimataifa

*Ni binti wa Malecela aliyetumbuliwa, ateuliwa kuwa bosi WHO

*Baba yake aeleza alivompigia simu usiku kumpa raarifa zilizomshangaza

Na MWANDISHI WETU

Mkurugenzi  wa zamani wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(Nimr), Dk. Mwele Malecela amateuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Shirika la Afya Duniani (WHO) katika kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya kitropiki  yasiyopewa kipaumbele (Neglected Tropical Disease).

Dk. Mwele anakwenda kutumikia nafasi hiyo ya juu katika kitengo hicho ambacho ni moja ya vitengo muhimu ndani ya WHO.

Kabla ya uteuzi wake, Dk. Mwele alikuwa  Mkurugenzi wa shirika hilo akisimamia vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, Kanda ya Afrika.

Akithibitisha kuteuliwa kwa Dk. Mwele, Waziri Mkuu mtaafu John Malecela ambaye ndiye mzazi wake, alisema anajivunia mafanikio ya binti yake.

Malecela alisema alipata taarifa hiyo kwa mshituko kwa sababu hakutarajia hivyo alifurahisha kwa mwanaye kuteuliwa katika nafasi hiyo na anamuombea kheri.

“Mwanangu alinipigia simu jana usiku(juzi) saa 4:30 na akaniambia taarifa hiyo njema, nilishituka sana.

“ Unajua watoto uliowalea, ukawasomesha na kadhalika wanapofauli katika maisha kwa vitu kama hivyo lazima ushituke na ufurahi,” alisema Malecela.

Aliongeza kwamba anafurahi zaidi kwa kumuona mwanaye popote alipo anawatumikia Watanzania na wanadamu wote kwa ujumla.

Taarifa za kuteuliwa kwa Dk. Mwele zilianza kusambaa juzi jioni kwenye mitandao ya kijamii ambapo watu mbalimbali waliandika ujumbe wa kumpongeza kwa kupewa nafasi hiyo.

Katika akaunti yake ya mtandao wa Twiter marafiki zake wengi walimpongeza huku naye aliwashukuru.

Akimshukuru mmoja wa marafiki zake  ambaye akaunti yake inautamburisho wa jina Thokopooley, Dk Mwele alisema; “ Asante sana Thoko, nimefurahi na kupokea heshima niliyopewa. Ninathamini na kukubali uteuzi wa kuongoza nafasi hii Dk. Tedros. Natarajia kufanya kazi pamoja nanyi ili kuendeleza mikakati ya kupambana dhidi ya magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele.

Rafiki yake mwingine ambaye akaunti yake inatambulishwa kwa jina la PeterHotez alimwandikia ujumbe uliosomeka kwamba ; “ Moyo umefurahi na unastahiri kupongezwa Dk. Mwele.Ni matarajio yangu kufanya kazi na kiongozi muhimu.

Fiona Fleming aliandika kwamba “ Wasichana hawawezi kuwa kwa kile wasichokona lakini sasa wanaweza kuona mwanamke kiongozi kwa vitendo! Ni habari ya kuvutia.

Dk. Mwele amemrithi Dk Dirk Engels ambaye amekiongoza kitengo hicho tangu Mei mosi 2014.

Dk. Mwele alitumbuliwa katika nafasi ya Ukurugenzi wa NIMR Rais Dk. John Magufuli Desemba 17 mwaka jana ikiwa ni siku moja baada ya kutoa ripoti ya utafisi wa magonjwa ndani yake ikiwamo taarifa ya virusi  vya ugionjwa wa Zika katika maeneo ya Morogoro, Geita na Magharibi mwa Tanzania.

Taarifa hiyo ilielezea kuwa kati ya watu 533 waliopimwa, asilimia 15.6 walibainika kuwa na virusi hivyo.

Dk MWELE NI NANI?

Dk. Mwele ameongoza taasisi mbalimbali za ndani na kimataifa, kwa sasa ni Mkurugenzi wa Tanzania Lymphatic Filariasis Elimination Program.

Ana shahada ya Sayansi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam,  Shahada ya uzamili na Uzamivu katika fani hiyo kutoka Chuo kikuu cha London (London (London School of Hygiene and Tropical Medicine).

Pia amewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu  NIMR kwa miaka 24, ambako alianza kazi akiwa mwanasayansi wa ngazi ya chini.

Akiwa Mkurugenzi wa NIMR aliimarisha taasisi hiyo, kupanua wigo wa utafiti na kuzitafsiri tafiti kwenye vitendo hususani sera na utekelezaji.

Pia amekuwa mstari wa mbele kuweka mikakati na kupigania shughuli za utafiti wa afya nchini Tanzania akiwa NIMR.

Dk. Malecela ni mwenyekiti wa

Kamati ya MRCC (Medical Research Coordinating Committee) na mewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika kamati za kimataifa.

Kwa sasa ni mshauri wa bodi ya taasisi ya Grand Challenges Canada na mjumbe wa idara ya afya katika Chuo cha Morhouse kilichopo nchini Marekani.

Pia ni mwanzilishi wa kikundi cha Imani kinachowasaidia watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).

 

 

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles