24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

NYOTA WALIOTIKISA USAJILI WA JANUARI

NA BADI MCHOMOLO


FAIDA kubwa ya dirisha dogo la usajili wa Januari barani Ulaya ni kuziba pengo la wachezaji katika kikosi kama wapo ambao wana majeruhi makubwa, sio lazima sana kufanya usajili katika kipindi hicho kwa kuwa usajili mkubwa tayari unakuwa umefanyika wakati wa majira ya joto.

Ligi inapomalizika wakati wa kiangazi timu nyingi zinafanya usajili wa nguvu kwa kuwa wanajua kile kichowafanya wamalize kwenye nafasi waliopo kwenye msimamo, hivyo usajili huo unaifanya klabu kuipa matumaini ya kuja kufanya vizuri kwenye msimu unaofuata.

Dalili za kuja kufanya vizuri zinaanzia kwenye mzunguko wa kwanza ambapo hadi Januari dalili hizo zinaonekana, hivyo kuanzia Januari mos hadi 31 klabu hizo zinafanya marekebisho ya kuongeza wachezaji wake.

SPOTIKIKI leo hii imekufanyia uchambuzi wa wachezaji ambao wametikisa katika kipindi hiki cha majira ya baridi au Januari.

Philippe Coutinho

Amekuwa mchezaji ambaye ametikisa usajili wa Januari mwaka huu kutokana na uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Barcelona ya nchini Hispania akitokea Liverpool ya nchini England.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ameweka historia mpya ya kuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa kwa fedha nyingi kutoka nchini England huku usajili wake ukikamilika kwa kitita cha pauni milioni 145, haijawahi kutokea.

Barcelona walikuwa wanaitaka saini ya mchezaji huyo tangu majira ya joto mwaka jana, lakini Liverpool hawakuwa tayari kumuacha mchezaji huyo aondoke, Januari hii Liverpool hawakuwa na namna kutokana na kiasi hicho kikubwa cha fedha kikiwa tofauti ni kile cha mwaka jana ambapo Barcelona waliweka mezani kiasi cha pauni milioni 100.

Lakini msimu huu mchezaji huyo alikuwa tayari kuondoka ili kuweza kutimiza ndoto zake za kucheza timu kubwa kama vile Barcelona, alifikia hatua ya kujinunua, yaani kuweka mezani pauni milioni 15 ili kuwapa Liverpool wamuache aondoke.

Van Dijk

Ni beki mpya wa kati wa klabu ya Liverpool, ambaye amesajiliwa kwa bei kubwa msimu huu nchini England hasa katika wachezaji ambao wanacheza nafasi za ulinzi.

Uhamisho wake umekamilika kwa kiasi cha pauni milioni 75, mchezaji huyo akitokea klabu ya Southampton, hata hivyo wapo ambao walipiga kelele kwamba mchezaji huyo amesajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha. Hata hivyo haijawahi kutokea kwa beki kusajiliwa kwa kiasi hicho kikubwa cha fedha.

Miongoni mwa watu ambao walipiga kelele kwa kushtushwa na usajili huo ni kocha wa klabu ya Man United, Jose Mourinho huku akidai kuwa na matumiza mabaya ya fedha.

Alexis Sanchez

Usajili wake umetikisa kwa kiasi kikubwa akijiunga na klabu ya Manchester United akitokea klabu ya Arsenal wakati huu wa Januari.

Mchezaji huyo anadaiwa kuwa anakuwa wa kwanza kwa kulipwa fedha nyingi kwa wiki akichukua pauni 350,000, hivyo kuwafunika wachezaji wote wanaokipiga katika Ligi ya England.

Arsenal walikuwa hawana namna ya kumzuia mchezaji huyo kubaki Emirates kwa kuwa mkataba wake ulikuwa unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Pierre Aubameyang

Ikiwa siku moja kabla ya kufungwa kwa usajili wa Januari, mchezaji huyo aliweza kutangazwa kuwa nyota mpya wa klabu ya Arsenal akitokea Borussia Dortmund kwa kitita cha pauni milioni 56.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alilazimika kufanya hivyo baada ya kumuuza mshambuliaji wake, Sanchez, hivyo kikosi chake kilikuwa na mapungufu makubwa katika safu ya ushambuliaji.

Kutokana na umahiri wake wa kupachika mabao, Arsenal wanaamini kuwa mchezaji huyo anaweza kuwapa furaha akishirikiana na wenzake.

Henrikh Mkhitaryan

Alikuwa nyota wa klabu ya Man United, amefanikiwa kujiunga na klabu ya Arsenal ikiwa kama sehemu ya kubadilishana na nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez aliyejiunga na United, usajili wake wametikisa sana Januari hii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles