24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Nyoso amtibua mdhamini Mbeya City

bin-slum-july25-2013NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

MMOJA ya wadhamini wa timu ya Mbeya City, Nassor Binslum, amelaani vikali udhalilishaji aliofanya beki wa timu hiyo, Juma Nyoso, kwa nahodha wa Azam FC, John Bocco.

Udhalilishaji huo wa Nyoso umemfanya kufungiwa kutoshiriki soka kwa miaka miwili pamoja na kulipa faini ya Sh 2,000,000.

Binslum anayeidhamini Mbeya City kupitia moja ya bidhaa zake za RB Battery, amesema juzi kuwa yeye binafsi na Kampuni yao ya Binslum Tyres Co Limited wanaunga mkono adhabu kali aliyopewa.

“Tunalaani tukio hilo kwa nguvu zetu zote kwa nahodha wa timu ambaye ndiye mwakilishi mkuu wa klabu, wadhamini pamoja na wananchi wa Mbeya kwa ujumla kwa tukio hilo alilomfanyia nahodha mwenzake wa Azam, John Bocco, ambalo ni tukio linalochukiza na sio tu kuuchafua mchezo wa soka bali pia kutuchafua sisi wadhamini na washirika wenzetu pamoja na wananchi wa Mkoa wa Mbeya,” alisema.

Binslum aliliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoa adhabu kama hizo kwa klabu na wachezaji wote nchini wenye tabia chafu huku akiwataka hata waandishi wa habari kufanya weledi huu huu waliotumia kutoa taarifa za unyama huo wa Nyoso.

“Kwani siamini mwenye tabia hizi chafu ni Nyoso peke yake bali wako wengi katika wachezaji wetu tena wengine wakichezea klabu kubwa zenye mashabiki wengi nchini, lakini hatujaona hata siku moja weledi huu uliotumika kumtia Nyoso hatiani ukitumika katika usawa ule ule kwa matukio ya aina ile ile,” alimalizia Binlsum.

Tayari uongozi wa Mbeya City umepinga uamuzi wa kufungiwa beki huyo kwa kukata rufaa TFF, ukidai kuwa hakupewa nafasi ya kusikilizwa na waliopelekea kufanya hivyo ni wachezaji wa Azam, John Bocco na Mudathir Yahya waliomchokoza.

“John Bocco alimpiga kibao usoni Christian Sembuli mbele ya mwamuzi, wakati Bocco akifanya hivyo, Mudathir alizunguka mgongoni kwa Bocco na kumvuta sehemu za siri (korodani) za Nyoso na akarudi upande wa kulia kwa mwamuzi, wakati Mudathir akifanya hivyo, Bocco alimkanyaga na kumpiga teke Nyoso,” ilisema sehemu ya taarifa ya Mbeya City.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles