27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Nyongo akemea unyanyasaji kwa wachimbaji wadogo wadogo

Ramadhan Hassan,Dodoma

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema  suala la unyanyasaji wa aina yoyote kwa wachimbaji wadogo wadogo  halikubaliki na mmliki yeyote atakaefanya hivyo atakuwa anavunja sheria  ya madini na za kazi.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Mei 21 bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Rhoda Kunchela (Chadema).

Katika swali lake Rhoda amedai kwamba sekta ya madini inaongeza pato kubwa katika uchumi wa nchi ambapo amehoji iwapo serikali ipo tayari kutatua kero kwa wachimbaji wadogo na vibarua ambao wananyanyasika katika migodi mbalimbali hapa nchini.

Akijibu swali hilo Nyongo amesema suala la unyanyasaji wa aina yoyote halikubaliki na mmliki yoyote atakaefanya hivyo atakuwa anavunja sheria  ya madini na za kazi.

Katika swali la nyongeza, Mbunge wa Mombo, David Silinde (Chadema) amehoji kuhusiana na kodi zinazotozwa kwa wachimbaji kuwa nyingi.

Akijibu, Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kodi ambazo zimefutwa na Bunge hakuna mbaye anatakiwa kutozwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yule ambaye atamtoza mchimbaji

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles