31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NYONGEZA YA MISHAHARA KUTOLEWA KIMYA KIMYA

Na ELIZABETH HOMBO – DODOMA


WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema kutangaza nyongeza ya mishahara ya watumishi wa umma hadharani, kuna athari zake kwa sababu kutaongeza mfumuko wa bei.

Amesema Serikali itaendelea kuongeza mishahara kimya kimya kama ambavyo inaendelea kulipa madeni ya watumishi wa umma.

Majaliwa, alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema), katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu.

Katika swali lake, Lyimo alisema tangu Serikali ya Awamu ya Tano, ilipoingia madarakani haijawahi kutoa nyongeza kwa watumishi jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Utumishi wa Umma.

Alisema hatua hiyo imechangia watumishi kukosa morali ya kufanya kazi, hivyo akahoji kwanini Serikali imewanyima haki hiyo ya msingi watumishi wake.

Katika majibu yake, Majaliwa alisema Serikali ina utaratibu kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, kuwapa stahiki watumishi wake kupitia Ofisi ya Rais, Utawala Bora.

Alisema ipo orodha ya watumishi wa umma ambayo imekamilika baada ya sensa ya kuwatambua watumishi na kazi inayoendelea ni uboreshaji wa nyongeza za mwaka, nyongeza za mishahara na upandishaji madaraja.

“Naomba niwaeleze watumishi wa umma waendelee kuwa na imani na Serikali kwa sababu mpango uliowekwa ni kuiwezesha Serikali kutolipa fedha nyingi kwa watumishi wasiostahiki.

“Pili baada ya kukamilika taratibu hizo, tumeshaanza kulipa madeni ya watumishi, nyongeza za mwaka zinaendelea kutolewa, lakini nyongeza za mishahara ni kile kilichozungumzwa na Rais John Magufuli kwenye sherehe za Mei Mosi, mwaka huu.

“Si kama Serikali haikusudii kuongeza mishahara kwa watumishi wake, lakini unapotumia Mei Mosi kutangaza nyongeza za mishahara, kunaleta athari kwenye jamii kwa sababu vitu vinapandishwa na kusumbua wananchi wasiolipwa mishahara.

Inaendelea…………… Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles