23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

NYAVU HARAMU ZA MIL 480/- ZAKAMATWA

Na EDITHA KARLO, KIGOMA

NYAVU haramu za uvuvi zenye thamani ya Sh milioni 480. 6, zimekamatwa katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuteketezwa kwa moto.

Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Emmanuel Maganga, wakati alipokuwa akishiriki uteketezaji wa nyavu hizo katika mwalo wa Kibirizi, mjini Kigoma.

Katika maelezo yake, Maganga alisema nyavu hizo zilikamatwa katika maeneo ya Kaseke, Muyobozi, Rwega, Mikamba na Rubufu kwa kushirikiana  na kitengo cha usimamizi na uthibiti wa uvuvi haramu.

“Nyavu zilizokamatwa na kuchomwa moto ni makokoro 66, monofilament 173, vyandarua 45, makila ya undersize 47, mitimbo mitatu, maboksi ya kuhifadhia samaki manane, kamba mita 22,500 na samaki wachanga kilo 720,” alisema Maganga.

Pamoja na hayo, mkuu huyo wa mkoa aliwataka wavuvi kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa ili kuhifadhi rasilimali ya uvuvi.

Naye Ofisa Mfawidhi Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi, Mkoa wa Kigoma, Rodrick Mbalimbali, alisema wameweka mikakati ya kudumu katika kukabiliana na upotevu wa mazao ya uvuvi ndani ya Ziwa Tanganyika.

Aliitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kusimamia sheria namba 22 ya uvuvi ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009 katika kupambana na zana haramu za uvuvi na mazao yasiyo na kiwango kinachokubalika.

“Mkakati mwingine ni wavuvi na wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi kuboresha vifaa vya kuhifadhia samaki pamoja na kukamilisha mitambo ya kuzalisha barafu.

“Upotevu wa ubora wa mazao ya uvuvi upo kwa aina zote za uvuvi ndani ya Ziwa Tanganyika, hivyo jambo hilo linaweza kupunguzwa kama nyenzo bora za uhifadhi zitapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu,” alisema Mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles