28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Nyalandu atahadharisha daftari la wapigakura

Ramadhan Hassan -Dodoma

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu ametaka uandikishaji wa maboresho katika daftari la wapigakura ufanyike kwa weledi na kutokuacha maeneo yenye wanachama wengi.

Nyalandu alitoa kauli hiyo juzi jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari.

 Alisema uandikishaji wa maboresho katika daftari la wapigakura unaoendelea, ufanyike kwa weledi na kutokuacha maeneo ambayo yana wanachama wengi wa chama fulani.

“Tunaomba wanaohusika waende kila jimbo, tarafa, kijiji, mtaa na kitongoji, wasiache mwanachama hata mmoja mahali ambako kuna wanachama wengi wa Chadema au CCM au vyama vingine, usitokee ufundi wa kukwepa yale maeneo kwamba hapa kuna wana Chadema wengi,” alisema.

Aidha Nyalandu alisema Serikali ijikite kuhakikisha inarekebisha mfumo wa uendeshaji wa elimu ya juu, sekondari na msingi.

“Elimu ya juu ijikite kwenye ubora ili vijana wetu wanaomaliza wawe na ushindani katika soko la ajira, ni lazima tuhakikishe mfumo unamwandaa kijana kuwa mshindani katika soko la ajira, ikiwa ni pamoja na kurekebisha mfumo wa utoaji wa mikopo katika elimu ya juu,” alisema Nyalandu.

Pia alitaka vijana ambao wapo katika vyuo vikuu wasifukuzwe vyuoni kwani wana ndoto nyingi katika maisha yao.

“Usimfukuze shule, usimkomoe, rekebisha mfumo, tatua tatizo sio kufukuza fukuza tu,” alisema Nyalandu.

Akizungumzia kuhusu kilimo, aliitaka Serikali katika kipindi hiki cha kilimo kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo zenye ubora.

“Sisi ni wakulima, nchi hii ni yetu sote, ningewaomba na kuwakumbusha katika kilimo wahakikishe wakulima wetu wote wanapatiwa pembejeo kwa wakati kwa sababu hizi mvua zitalihakikishia taifa usalama wa chakula,” alisema Nyalandu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles