29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

NUSU FAINALI KIKAPU HAPATOSHI TAIFA

NA SHARIFA MMASI

HATUA ya nusu fainali ya mashindano ya kombe la StarTimes ‘StarTimes Super Cup’, imepangwa kuendelea leo kwa michezo miwili kuchezwa kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa awali kwa siku hiyo utakaonguruma  jioni, utaikutanisha timu ya Savio dhidi ya Oilers, ukifuatiwa   JKT na Tanzania Prisons.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha wa Savio, William Mziray, alisema wachezaji wake wamejipanga vema kuibuka kidedea katika mchezo huo.

“Tunamshukuru Mungu kwa kutupa nguvu na kuweza kufanya vema tangu kufunguliwa kwa mashindano haya.

“Kuelekea mchezo wetu wa kesho (leo), wachezaji wangu wote wapo katika hali ya ushindani, kila mchezaji ana morali ya juu hivyo naamini watacheza kwa viwango ili tuibuke na ushindi,” alisema Mziray.

Kwa upande wake kocha wa JKT, Alfred Ngalaliji, alisema hawana hofu yoyote na wapinzani wao Tanzania Prisons hivyo lazima wawafunge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles