NONDO AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

0
632

 

|Francis Godwin, IringaMwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo anayekabiliwa na mashtaka ya kusambaza taarifa za uongo akidai kutekwa amekutwa na kesi ya kujibu.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Agosti 27, na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa,  Liad Chamshama baada kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka.

Hakimu Chamshama amesema kutokana na uamuzi huo, Nondo anatakiwa kujitetea dhidi ya mashtaka yanayomkabili ambapo anatakiwa kujitetea.

Nondo anatarajia kuleta mahakamani mashahidi wasiopungua watano kutoa ushahidi katika kesi yake hiyo ambayo imepangwa kusikilizwa kati ya Septemba 18 na 19, mwaka huu.

Nondo ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kabla hajasimamishwa masomo kutokan ana kesi hii, anadaiwa kusambaza taarifa za uongo akiwa jijini Dar es Salaam kuwa ametekwa na shtaka la pili anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwa polisi katika Kituo cha Mafinga mjini Iringa.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here