NMB Private Banking inasisitiza dhana mteja  mfalme

0
690

Na Shermarx Ngahemera

EUROMONEY ni jarida la masuala ya huduma za kifedha duniani  linalochapishwa  nchini Uingereza na kwa miaka mitano mfululizo limekua likiiteua Benki ya NMB Plc kuwa benki bora nchini  kwa huduma zake sio kwa hiyana bali kwa hali na mwenendo wake unaofanya kila mmoja alipo kuwa mhusika wa benki hiyo.

Wateja wa NMB Plc hufaidika na huduma za kipekee za Private Banking kwa kupitia matawi yake mahsusi ya  kibenki yatoayo  huduyma hiyo adhimu kibenki.

Kwa kuwa Benki ya NMB Plc inafanya huduma za rejareja kamili  (Retail banking ) ina wateja zaidi kuliko benki nyingine yoyote nchini na huduma zake zimefika hadi katika kila wilaya kwa kuweko na tawi lake.

Kisha kuwa na miundombinu  sahihi (kwa kuangalia na kujisikia) ya matawi ya benki, teknolojia ya  kisasa , imefuta foleni ndefu  katika kupata bidhaa na huduma ambazo hazikuonekana kupendelewa  na Watu wa Kipato kikubwa (High Net Worth s au HNWIs) na hivyo kudai huduma bora zaidi.

Hivi basi huduma binafsi, (Private Banking ) ni jibu kwa mahitaji ya kuwepo huduma maridhawa kwa wateja.
NMB  ina imani kuwa mwenendo wa ukuaji wake wa soko ni wa hali ya juu kati ya taasisi nyingine za fedha. Kuna bidhaa za hali ya juu na kwa kutumia huduma  za teknolojia mpya kama vile intaneti yaani huduma mtandao,  Simu janja , Private Banking, MasterCard na Visa na mtandao wa Wakala ni jibu kwa matatizo mengi ya wateja.
Benki hiyo inaamini kuwa uanzishwaji wa Benki ya Binafsi ni muhimu sana na vituo vya Biashara (Business Clubs) kwani  kihistoria maboresho mengi yamefanyika kuanzia mwaka 2014, kwa  NMB kuimarisha  vituo vyake vya  kibenki na biashara ili kutoa huduma za kibinafsi zaidi ambazo zinajenga urahisi na  kuwa benki ya kipekee.

Kuna  mameneja wa uhusiano ili kuhakikisha wateja wawe na kipaumbele kikubwa, kupewa kinachostahili mahitaji yao na maisha yao kwa dhana kamili ya kuwa mteja ni mfalme.

Huduma za pekee

Katika matawi ya benki binafsi na vituo vya biashara, NMB husaidia wateja kutambua malengo yao ya kifedha kwa wakati kwa kuwa mshirika katika maendeleo yao, na kutoa upekee, urahisi,  na wateja wana fursa ya kujiunga na programu za Titanium Debit MasterCard  ambazo zinazo faida kadhaa  na kutambuliwa kwao ulimwengu mzima.

Faida hizi zinapanuliwa kwa wanachama wa familia na benki mara zote hupokea  simu za  watu hao mashuhuri (VIP).

Isitoshe Uzoefu unaopatikana  kwa mfumo huu wa pekee unatoa nafasi ya upatikanaji wa mikopo ya upendeleo na masharti  bora ya amana pamoja na viwango rafiki vya ubadilishaji wa fedha za kigeni.

NMB inajitahidi kutoa huduma bora kupitia usimamizi bora wa akaunti ya mteja. Maelezo ya Huduma Binafsi (Private Banking ) yana harufu  nzuri iliyojengwa  ili kuwafikia wateja wa Benki wa kipato kikubwa  na malengo makubwa ambao mahitaji yao ni ya zaidi ya benki ya kwaida na hivyo hushughulikia katika  mfumo wa mtu na mahitaji yake mahsusi kwa wakati anaopenda yeye mteja. NMB Plc hupendelea changamoto hizo kwa imani kuwa mteja kwao ni mfalme.Mambo muhimu yanayopatikana  na kuvuna ni Huduma za kibinafsi zaidi, urahisi usio na vikwazo  na gharama  zisizo hasara na kupewa tuzo za kipekee.

Kwa kuzingatia upekee wa huduma hizo Binafsi hutolewa katika matawi yake mahsusi na Vituo Vya Biashara kwenye mikoa ambako hakuna matawi ya Private Banking ; kwa sasa matawi rasmi ni yale ya

Benki  NMB  matatu yakiwamo  NMB Oster Plaza, NMB Ohio na NMB Bunge ambapo wateja hapo hutumikiwa kwa kupitia Mameneja wa Uhusiano.

Isitoshe  katika hali ambapo mteja wa Benki ya Kibinafsi anatembelea matawi yetu ya kawaida kwenye mtandao, watatambuliwa na ulimwengu wa asili na Titanium MasterCard iliyotolewa kwao na kutumikia kwa njia ya dirisha la Mwongozo wa Fast Track kwenye mtandao wa Tawi la NMB nchini kote. Ni raha tupu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here