25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

NMB Kuwawezesha wakulima kulima kisasa

DERICK MILTON-SIMIYU

Benki ya NMB nchini imesema kuwa itahakikisha inaendeleza jitihada zake za kuhakikisha wakulima wanawezeshwa kadri wanavyohitaji kulingana na mazao yao na kuifanya sekta ya kilimo kubeba uchumi wa nchi.

Mbali na hilo benki hiyo imesema kuwa kwa muda mrefu imekuwa ikitangaza na kuwasaidia wakulima kama ajenda yake kuu, kutokana na asilimia kubwa ya watanzania kutegemea sekta hiyo.

Hayo yamesemwa leo Meneja wa benki hiyo Kanda ya Magharibi, Sospeter Magesse, wakati akikabidhi kiasi cha sh. Milioni 30 kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini, kama udhamini wa benki hiyo kwenye maonyesho ya sikukuu ya wakulima (Nanenane) kitaifa yanayofanyikia Mkoani humo.

Amesema katika maonesho hayo benki hiyo imejipanga kuhakikisha inatoa elimu kwa wakulima na wafugaji jinsi ya kulima kisasa na kitaalamu ikiwa ni pamoja na kuwaeleza jinsi gani benki hiyo inaweza kushiriki kwenye kilimo kwa kuwapatia mikopo.

“Kwenye maonyesho ya mwaka huu ambayo yatakuwa bora zaidi, ushiriki wetu kama benki utakuwa mkubwa zaidi, na umelenga kuwasaida wakulima, tutakuwa na bidhaa za wafugaji wa ng’ombe, na wakulima wa mazao ya pamba, tumbaku na kahawa lakini hata Matrekta tutakuwa nayo,” amesema Magesse.

Akiongea mara baada ya kupokea mchango huo, Katibu Tawala huyo ameishukuru benki hiyo kwa mchango wake, ambao amesema utawezesha kuboresha zaidi eneo ya Nyakabindi ambako sherehe hizo zinafanyika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles