33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Nkasi aagiza walimu wanaokacha kufundisha msimu wa masika wachukuliwe hatua

 

Gurian Adolf, Nkasi



Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda amewaagiza waratibu elimu kata kuanza mkakati wa kuwachukulia hatua walimu ambao wamekuwa na tabia ya kuacha kazi yao ya kufundisha nyakati za masika na badala yake kujikita katika shughuli za kilimo.

Agizo hilo alilitoa juzi wakati akizungumza na waratibu elimu kata wakati akikabidhi pikipiki 28 zenye thamani ya Sh milioni 98 zilizotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa ajili ya mpango wa kukuza  stadi za kusoma kuandika na kuhesabu kwa waratibu kata wa wilaya hiyo.

“Kila unapofika msimu wa masika kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakiacha jukumu lao la msingi waliloajiriwa na serikali la kufundisha na kujikita katika kilimo kitendo kinachosababisha wanafunzi wakose haki yao ya kupata elimu,” amesema.

Mtanda alisema kuwa miongoni mwa kazi za waratibu elimu kata ni kuhakikisha kuwa walimu wanakuwepo shuleni  muda wote  wa masaa ya kazi sambamba na kufundisha bila kutegea.

“Nawaagiza waratibu elimu hakikisheni mnapita katika shule zilizopo katika kata zenu na kukagua kama walimu wanawajibika, kwa kuwa hivi sasa serikali imewapa nyenzo ya kuwawezesha kutembelea shule mnazozisimamia,” amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Misana Kwangula amesema lengo la serikali kutoa pikipiki hizo ni kuwawezesha waratibu elimu kuzunguka katika shule wanazozisimamia ili waweze kutatua changamoto zilizopo katika shule hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles