Imechapishwa: Tue, Sep 12th, 2017

NIYONZIMA, OKWI WAYEYUKA MAZOEZINI SIMBA

 

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI Emmanuel Okwi na kiungo, Haruna Niyonzima, jana walishindwa kufanya mazoezi na wachezaji wengine wa Simba kutokana na kusumbuliwa na maradhi.

Kikosi cha Simba kinaendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kikijiandaa na mchezo wake ujao dhidi ya Mwadui FC  utakaofanyika wikiendi hii.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe, aliliambia MTANZANIA jana kuwa waliwatarajia wachezaji hao wangejumuika na wenzao mazoezini lakini walishindwa baada ya kila mmoja kutoa taarifa ya kuugua.

“Niyonzima (Haruna) alifika hapa asubuhi na kuniambia anasumbuliwa na tumbo hali hiyo ilisababisha ashindwe kufanya mazoezi.

“Tumempa mapumziko lakini ataungana na wenzake kwenye mazoezi ya kesho (leo) jioni,” alisema Dk. Gembe.

Kuhusu Okwi, Gembe alisema mshambuliaji huyo alimpigia simu asubuhi na kumpa taarifa kuwa anasumbuliwa na kichwa, lakini ataungana nao kwenye mazoezi ya leo.

“Okwi alikuwa ahudhurie mazoezi na wenzake leo, lakini asubuhi alinipigia simu kuwa ameamka kichwa kinamuuna na yeye ameshindwa kuja badala yake ataendelea na mazoezi kesho jioni kama atakuwa fiti,” alisema.

Weka maoni yako

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>

YOUTUBE

NIYONZIMA, OKWI WAYEYUKA MAZOEZINI SIMBA