Nikki wa Pili aanika msoto aliopitia

0
585

Na GLORY MLAY

MSANII wa Hip Hop nchini, Nickson Simon maarufu Nikki wa Pili, amesema maisha ambayo ameyapitia akiwa bado mdogo, ndio sababu inayomfanya azidi kufanya makubwa kwenye maisha yake ya kawaiada na muziki.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Nikki wa Pili alisema alipitia changamoto nyingi ikiwemo kuuza sambusa kwenye vilabu vya pombe akiwa na umri mdogo.

“Nilikuwa nauza sambusa kwenye vilabu vya pombe, kila siku nilikuwa nazunguka na sambusa zangu, nimefanya hivyo tangu nipo darasa la tatu mpaka namaliza la saba lakini kupitia changamoto hizo zilizotufanya tufanye makubwa zaidi,” alisema Niki wa Pili.

Alisema kila mmoja anajukumu la kuhakikisha haongezi matatizo bali anapambana kuyapunguza maana kwenye matatizo ndipo wanapotokea hivyo wasanii na vijana wasikate tamaana kutokana na changamoto wanazopitia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here