NICKI MINAJ AMHOFIA SAFAREE, AONGEZA WALINZI

0
549

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Nicki Minaj, ameongeza walinzi wake kwa kumhofia aliyekuwa mpenzi wake, Safaree Samuels.

Nicki na Samuels walikuwa kwenye uhusiano kwa kipindi cha miaka 15 kabla ya kuachana, kwa sasa wawili hao wameingia kwenye mgogoro, jambo ambalo linampa Nicki wasiwasi wa maisha yake.

Mrembo huyo ameachia albamu yake mpya ijulikanayo kwa jina la Queen, hivyo amekuwa akitumia muda mwingi kwa ajili ya kufanya ziara ya habari ili kuzidi kuitangaza albamu hiyo, kutokana na hali hiyo ya kutembea kwenye radio na TV mbalimbali, ameamua kuongeza walinzi wa kumlinda.

Hata hivyo, Samuels kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka wazi kuwa hana mpango wa kurudiana na mrembo huyo na hana mpango wa kufuatilia maisha yake kama anavyodhani, lakini mitandao ya kijamii itaendelea kuwafuatilia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here