NICK AMZAWADIA WIMBO PRYANKA CHOPRA

0
471

NEW YORK, MAREKANI


BAADA ya wiki moja iliyopita mastaa wa filamu na muziki, Nick Jonas na mpenzi Priyanka Chopra, kutambulishana kwa wazazi, sasa Nick ameamua kumpa zawadi ya wimbo mpenzi huyo.

Wiki moja iliyopita, Priyanka alimwomba Nick kwenda na wazazi wake mjini Mumbai kwa ajili ya kutambulishana na ikadaiwa kwamba wawili hao walifungishwa ndoa ya kijadi kwanza kutokana na utaratibu wa familia ya mrembo huyo.

Kitendo hicho kimemfanya Nick aamini kuwa Priyanka ni mali yake, hivyo ameamua kuachia wimbo mpya ambao unajulikana kwa jina la ‘Right Now’ ukiwa unazungumzia maisha ya mapenzi yake kwa mrembo huyo.

Hata hivyo, baada ya kuachia wimbo huo, Nick alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuandika ‘Wewe ni maji yangu, jua langu, mwezi na nyota zangu, moyo wako ndio kitu ninachokitaka’, maneno hayo pia yapo kwenye wimbo wake huo mpya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here