27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

NIC YATAKA WAFUGAJI WAJIUNGE NA BIMA

NA HARRIETH MANDARI


WAFUGAJI nchini Tanzania wametakiwa kukatia bima mifugo yao  na kuachana na utamamduni wa kumiliki mifugo mingi  ambayo linapotokea janga hufa na hivyo kumwacha mfugaji kupata hasara.

Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Sam Kamanga, ameliambia MTANZANIA wikiendi iliyopita Dar es Salaam wakati akielezea mikakati ya NIC kwa mwaka huu, akatolea mfano wa  wamiliki wa ng’ombe walio wengi nchini bado ni  wachungaji ng’ombe na si wafugaji kama dhana ilivyozoeleka na wengi.

Akafafanua kuwa kufuga ni hali ya kumiliki mifugo ambayo hupata mahitaji yote wakiwa sehemu moja na si  kuswaga ng’ombe mwendo mrefu kupata malisho.

“Shirika la NIC limedhamiria kwa mwaka huu kuhakikisha kuwa tunatoa elimu kwa Watanzania wanaomiliki ng’ombe wengi  na wakati huo huo hawana uwezo wa kuwapatia malisho bora, badala yake wageuke na kuwa wafugaji kwa kuwa na ng’ombe wachache (Zero grazing) ambao watapatiwa malisho katika eneo moja bila kubughudhi makundi mengine kama wakulima,” alisema.

Mwamanga alisema Watanzania wengi wanazifahamu huduma chache sana za bima zikiwemo za magari na afya, lakini kuna  nyingine muhimu zikiwemo; bima za moto, elimu, maisha, mafuriko, tetemeko na nyingine nyingi.

Akatolea mfano wa makundi muhimu katika uzalishaji kama vile wavuvi na wakulima, alisema ni vizuri huduma hizo ziwafikie kikamilifu ili nchi ipate maendelelo kwa kasi.

Aliongeza kuwa Watanzania wanatakiwa waepukanae na dhana kuwa kujiunga na bima ni kwa ajili ya wenye kipato kikubwa tu, jambo ambalo si kweli kwani hata mtu wa kipato cha chini ana uwezo wa kujiunga na akanufaika kwa kiasi kikubwa.

“Wengi wanafikiri bima ni za bidhaa  kama magari, kumbe huduma hiyo ni kwa mambo mengi, hata kwa wakulima pia ni muhimu ambapo mkulima anatakiwa kukata bima kama dhamana ya kujipatia mkopo kwa nia ya kuboresha kilimo na hivyo kuweza kuwa mkulima bora na si bora mkulima,” alisema.

Alizitaja baadhi ya bima za wakulima zikiwemo za mazao, bima za vifaa vya kilimo na  bima za pembejeo ambapo mkulima anapata  mkopo kwa urahisi kutoka mabenki ikiwemo Benki ya Maendeleo ya TADB na kutumia bima yake kama dhamana.

 Hivi sasa kumekuwa na migogoro mingi isiyokwisha baina ya wakulima na wafugaji. Wengi wao ni wa  jadi ambao mifugo yao mingi (asilimia 48) huhama hama wakitafuta malisho na maji.

Ufugaji wa kuhamahama ni chanzo cha migogoro mikubwa nchini. Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi hivi sasa kuna kaya 15,488 au asilimia wanaoendelea na aina hiyo ya ufugaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles